Na Mwantanga Ame
VITUO vilivyoanzishwa kwa ajili ya kusaidia huduma maarufu kama ‘One Stop Center’, vimetajwa kuwa haviifaidishi serikali, bali huwasaidia zaidi watendaji wanaopewa vituo hivyo.
Wadau na wafanyabiashara wa Zanzibar walieleza hayo kwenye warsha iliyofanyika hivi karibuni katika hoteli ya Grand Palace iliyopo Malindi mjini hapa.
Baadhi ya wafanyabiashara hao walieleza kuwa vituo vya ‘One Stop Center’ viliovyopo havionekani kuleta tija kwa wananchi bali vimekuwa vikiwajengea mazingira mazuri ya maisha watendaji wanaosimamia vituo hivyo.
Khamis Nassor Msimamizi wa Chama cha Ogani, alisema nia ya serikali kuweka vituo vya ‘One Stop Center’, ni kusaidia kupunguza urasimu wa upatikanaji wa huduma hasa katika kusajili miradi lakini ziliopo hazifanyi kazi vizuri.
Akitoa mfano alisema katika ‘One Stop Center’ ya uwekezaji bado tatizo limekuwa kubwa kwani watu wanachukua muda mwingi kusajiliwa miradi yao kiasi ambacho huwasababishia kuviona vituo hivyo havina maana.
Alisema hali hiyo imekuwa ikiwafanya kushindwa kuwa na viwango bora vya kuanzisha miradi kutokana na baadhi ya watendaji kugeuza urasimu sehemu ya manufaa yao binafsi.
Alisema inawezekana kukuwa kwa tatizo hilo kunasababishwa na wengi wa watendaji wanaowekwa katika vituo hivyo kukosa sifa za moja kwa moja kupitisha maamuzi juu ya mradi wowote kwa vile mengi ya mambo ya serikali hupitishwa na makatibu wakuu.
“Hapa kwetu Katibu Mkuu ndio wanaotoa maamuzi sasa hawa wanaowekwa katika vituo vya ‘One Stop Center’ hawana nguvu yoyote hadi liende kwa katibu Mkuu sasa anaposafiri umsubiri hadi arudi sasa hapa ndipo panapotokea rushwa”, alisema Khamis.
Alisema inawezekana serikali ikaunda vituo vingi vya ‘One stop Center’ lakini ikajikuta havileti manufaa kutokana na mfumo huo uliopo sasa kwani kilichotakiwa serikali kuwapa nguvu ya kufanya maamuzi bila ya Makatibu Wakuu ambapo wao wanatakiwa kubaki kama wasimamizi.
Alisema suala la elimu ya Juu katika utafiti uliowahi kufanywa kwa upande wa elimu ya Juu, hali ni mbaya matumizi ya teknologia ipo nyuma, miundombinu bado sio mizuri na matumizi ya pesa katika ubunifu hali sio mbaya lakini kwa bahati mbaya zaidi hali sio nzuri kwa makampuni ndogo ndogo huku kampuni kubwa zikiwa zinafanya vizuri.
Akiendelea alisema ili kuweza kusajili mradi na kuweza kufanya biashara yako katika utafiti huo alisema Tanzania hudukua siku 29 wakati nchi jirani huchukua siku mbili huku kuweza kupata kibali kwa Tanzania huchukua siku 308 kulipa kodi siku saba na kufunga biashara siku 1000.
Alisema hali hiyo sio nzuri na ni vyema serikali ikabadilika kuona inarahisisha shughuli zake kwa kuwa na vituo vya ‘One Stop Center’ ambazo zitawawezesha wafanyabiashara kuzitumia kumaliza mahitai yao kwa haraka.
No comments:
Post a Comment