Habari za Punde

MIGOGORO 73 YA ARDHI HAIJATOLEWA HUKUMU

NAIBU Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati, Haji Mwadini Makame amesema kiasi ya migogoro 17 imeweza kutatuliwa na migogoro 73 haijatolewa hukumu kutokana na kuchelewa kuteuliwa kwa mahakimu katika mahkama za mikoa.

Alisema Serikali iko mbioni kutoa elimu kwa wananchi ili kuondoa matatizo mengi yanayotokana na matumizi ya ardhi.

Aidha alisema vile vile watafanya mapitio ya sheria ya ardhi na sera ya ardhi ili kuwasaidia wananchi kuwa na uelewa wa masuala ya ardhi.

Hayo aliyasema alipokuwa akijibu suali la Mbarouk Wadi Mussa (Mkwajuni), aliyetaka kujua Serikali inampango gani wa kuweza kuwasaidia wananchi ili kuondokana na tatizo hilo.

Waziri alikiri kuwa migogoro ya ardhi imekuwa mingi tafauti na zamani kwa sababu ardhi imekuwa na thamani kutokana na uwekezaji ,hivyo wananchi wananchi wengi wameelewa thamani ya ardhi kutokana na uwekezaji tafauti na zamani.

Aidha alisema ongezeko la watu na kukuwa kwa shughuli mbali mbali za kijamii imechangia kuibuka migogoro mbali mbali ya ardhi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.