WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, imesema ni kosa kwa walimu kuwasitishamasomo wanafunzi kwa kukosa ada licha ya wizara kutoa mwongozo kuwataka wazazi kuchangia huduma za kielimu.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi huko, ofisini kwake Chake Chake Pemba, Mratibu Mipango, Sera na Utafiti wa Wizara hiyo,Khamis Salum Mohamed , alisema wizara kweli ilitowa mwongozo wa michango hiyo lakini haijatoa tamko ambalo linawaruhusu walimu kuwasitisha masomo wanafunzi kwa mudakwa kukosa michango.
Alielezakuwa wizara inawataka walimu kutafuta mbinu za kupata michango hiyo, kwa kushauriana na kamati za skuli lakini sio kumsitisha masomo mwanafunzi kwanikufanya hivyo ni kosa kisheria.
Alisema kamati za skuli zina mamlaka kwa mujibu wa muongozo huo namba10 wa 1999, kubadilisha viwango vya michango kulingana na mazingira ili zisiwakwaze wazazi katika uchangiaji.
Alifahamishakuwa mwongozo huo, umeweka viwango vya malipo ya michango hiyo kwa skuli za maandalizimijini kwa mwaka shilingi 2,500 kwa mtoto mmoja, msingi kuanzia darasa la kwanza hadi saba shilingi, 7,3000, sekondari kidato cha kwanza hadi cha pili shilingi 5,000 kwa kila mwanafunzi kwa mwaka.
Aliongezakusema kidato cha tatu hadi nne (7,500) na kidato cha tano hadi sita pamoja na mafunzo ya ufundi ni shilingi 10,000 kwa mtoto kwa mwaka, wakati mafunzo ya ualimu cheti ni shilingi 15,000 na mafunzo ya ualimu stashahadani shilingi 20,000.
Alisema kusitishwa masomo kwa baadhi ya wanafunzi wanaoshindwa michango, Wizara haina taarifa juu ya suala hilo.
Aidha alisema ni vyema zikatumika busara nyengine za kupata michango hiyo kwa kuwaita wazazi wa wanafunzi ili kuwaeleza na kutafuta uwezekano wa kupata michango hiyo.
Afisahuyo alisema walimu hawawezi kuzidisha viwango kwa vile wana udhibiti wa kamaliza skuli kwa maana hiyo kinachotozwa ni idadi ile ile iliyoidhinishwa katika mwongozo huo.
Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi, umebaini kuwa kuna baadhi ya wanafunzi walifaulu michepuo na kuanza masomo yaokatika skuli walizopangiwa lakini wazazi waliamua kuwarejesha skuli walizotokakwa kutomudu gharama za uchangiaji.
Uchunguzihuo pia ulibaini kuwa pamoja na kiwango hicho kuelezwa ni kidogo lakini kuna baadhi ya wazazi wanao watoto zaidi ya wawili ambao wanatakiwa kulipiwa ada wakati uwezo wao ni mdogo.
No comments:
Post a Comment