SMZ kununua mashine ya DNA
NAIBU Waziri wa Afya, Dk. Sira Ubwa Mamboya, amesema Serikali ina mpango wa kununua mashine ya DNA kutokana na umuhimu wake.
Alisema mpaka sasa Serikali imeshafanya upembuzi yakinifu kwa kushirikiana na ofisi ya maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ya Muungano, pamoja na kutayarisha jengo la Mkemia Mkuu kwa ajili ya kuweka mashine hiyo.
Dk. Sira alisema hayo katika kikao cha Baraza la Wawakilishi alipokuwa akijibu suali la Fatma Mabrouk Said (Amani), aliyetaka kufahamu Serikali ina mpango gani wa kupatikana kipimo hicho hapa nchini.
Aidha alisema DNA ni mashine ya kupima uasilia pale panapotokezea utata wa mtoto, kipimo hicho hufanyika baada ya kuzaliwa mtoto na kuthibitisha nani baba halisi.
Sambamba na hayo alisema suala la kuwapa mimba wasichana ni ukosefu wa maadili na hakuna uhusiano na ukosefu wa mashine hiyo.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Wapatiwa Mafunzo Elekezi
-
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameshiriki
katika Mafunzo elekezi kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar
yanayofany...
1 hour ago

No comments:
Post a Comment