VIONGOZI wa meza kuu wakisimama kwa dakika moja kumkmbuka Mwanamichezo Khamis Shaban. ambaye amekuwa mdau mkubwa wa habari za michezo katika Redio Zanzibar.
MGENI rasmin akiwa katika picha ya pamoja na wanamichezo waliotunukiwa zawadi na Taswa Zanzibar katika ukumbi wa Hoteli ya Ocein View Kilimani.
MFANYABIASHARA na Mwanamichezo Zanzibar Mohammed Raza mdhamini wa sherehe hiyo akitowa nasaha zake kwa Wanamichezo na Waandishi wa habari kwa kufanikisha shughuli hii ya kuwazawadia zawadi wanamichezo wa Zanzibar.
MWENYEKITI wa Taswa Zanzibar Mwinyimvua Abdi. akitowa maelezo katika sherehe za kuwazawadia zawadi Wanamichezo wa Zanzibar waliofanya vizuri michezo ya Riadha ya Zone 5 yaliofanyika Dar- es- Salaam.
KATIBU wa Taswa Zanzibar Donisia Thomas akiwaidi wanamichezo katika serehe za kuwatunuku mazawadi yalioandaliwa na Wanahabari za Michezo( Zanzibar Taswa)
MAKAMU Mwenyekiti wa Taswa Zanzibar Maulid Hamad akielezea umuhimu wa Wanamichezo katika kuliletea Taifa heheshima ya ushindi katika michezowakati wa kuwatuniku zawadi walengwa hao wa mchezo wa riadha.
NASRIA Hashir ni mshindi wa mbio za mita 100 akikabidhiwa medali yake na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika mashindano ya Zone 5 yaliofanyika Dar -es - Salaam.
WADAU wa michezo Zanzibar wakijumuika katika sferehe za kuwatunukia zawadi washindi hao katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocein View Kilimani.
AHMAD Bakari akipongezwa na Mkuu wa Mkoa wa Mji Magharibi kwa kuwa mshindi wa kwanza katika Vijana Olimpiki Maalum na kujinyakulia medali ya Dhahabu.
BAADHI ya Wanamichezo wakijumuika na Washindi wa Mbio za Riadha walioshiriki mashindano ya Kimataifa ya Zone 5 yalifanyika Dar -es- Salaam.
AHMAD Bakari ni mmoja wa mwanariadha wa Zanzibar alishinda mita mia nne dhahabu kwa upande wa Vijana ya Olimpiki Maalum yaliofanyika Ugiriki.
No comments:
Post a Comment