Habari za Punde

JESHI LA POLISI BANDARINI WAKAMATA PEMBE ZA TEMBO ZIKIWA KATIKA KONTENA KWA KUSAFIRISHWA NJE YA NCHI


Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar ACP. Muhud Mshihiri akizungumza na wakala wa kusafirisha mizingi na msimamizi wa mzingo huo, wakati wa zoezi la kuendelea kupekuwa magunia ya Dagaa ikiwa ndani yake mmeweka Pembe za Tembo, kulia Kamanda wa Polisi Marine Zanzibar SP Martin Lissu.   

 Mkuu wa Kikosi cha Polisi Bandarini Zanzibar SP Martin Lissu akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio bandarini Zanzibar wakati wa zoezi likiendelea. 

 MMOJA ya Konteni lilokuwa likisubiri kusafirishwa na kago ya magunia ya Dagaa na kuchanganywa na Pembe za Tembo likiwa katika upekuzi baada ya kugundulika kuwa na Nyara za Serikali zikitaka kusafirishwa nje ya Nchi.  

 HIVI ndivyo ilivyokuwa kufunguwa kila gunia kutowa kisicho husika katika magunia ya Dagaa inayosemekana yakitokea Mwanza na kusafirishwa nje kupitia bandari ya Zanzibar. 

 KIPUSA kikitolewa katika magunia ya dagaa wakati wa zoezi hilo likiendelea katika bandari ya Zanzibar.


 ASKARI  wa Kituo cha Pilisi Bandari wakihakikisha hesabu ya kinachotolewa katika upekuzi huo kinakuwa sawa
 HIVI ndivyo ilivyokuwa jinsi ilivyohifadhiwa

 ASKARI wa Kikosi cha Kuzuia Magendo KMKM akihakikisha kila gunia kujuwa kilichomo ndani katika zoezi hilo.   
ZOEZI likiendelea chini ya ulinzi mkali wa vyombo husika katika bandari ya Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.