Habari za Punde

MAALIM MUSSA KHAMIS AAGWA BARAZA LA WAWAKILISHI


Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi walipokuwa wakiuaga mwili wa Marehemu Maalim Mussa Khamis Silima baada ya kufikishwa katika Ukumbi wa Baraza.

Kwa mujibu wa kanuni za Baraza mwakilishi yeyote atakaefariki atapaswa kufikishwa katika Baraza kwa ajili ya kuombewa dua na Jeneza kufunikwa Bendera ya Baraza la Wawakilishi.

Mazishi ya Maalim Mussa yalifanyika leo huko kiijini kwao Kiboje.

3 comments:

  1. Mimi hapa nitapingana na kanuni hii kwa sababu.

    Suala hili ni la kidini zaidi kwa hivyo taratibu za kidini ndizo zifanye kazi. Na katika taratibu za kidini hakuna suala la kufunikwa bendera wala maiti kupelekwa sehemu kwenda kuagwa hasa ikiwa ni maiti ya kiislamu.

    Kama tunaiga mambo tujaribu kuangalia kwanza kwenye asili yetu, mila zetu kama waislamu na hadhi yetu mengine yatatupeleka pabaya.

    Wallaahu A'alamu

    ReplyDelete
  2. Ndugu yangu tuache kucomplicate mambo, suala hili halina ubaya kama unavyofikiria, kwani suala la mazishi ukitoa yale mambo ya lazima jamii nyingi za waislamu zimetofautiana mfano, warabu hata jenenza hawafuniki wengine wanaweka mapicha na mauwa mfano jamii za eastern europe:kosovo,albania etc russia mfano chechnya,azabeijan etc acha hizo! uislamu mwepeeeai wallah!

    ReplyDelete
  3. Ndugu yangu Adhubany hatupo katika kucomplicate mambo bali tupo katika kufahamishana.

    Kama ni Muislamu unafahamu fika kwamba Muislamu akifariki basi taratibu za dini yake ndiyo zinazofuatwa wakati wa maziko.Na taratibu hizi ziko very clear na nadhani kuanza kuleta mambo ya aina hii ndiyo tunaanza kucomplicate kwani mwengine atakuja na jengine na kuendelea. Kama na Suala la kidini acha sheria ya dini ifanye kazi na si vyenginevyo.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.