Habari za Punde

KAZI YA KUOPOA MIILI KATIKA MABAKI YA MELI ILIYOZAMA BADO NI NGUMU

Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi- Zanzibar

ZANZIBAR JUMATANO SEPTEMBA 14, 2011. Wazamiaji kutoka nchini Afrika ya kusini kwa kushirikiana na wazamiaji wa Jeshi la Wananchi WA Tanzania JWTZ, Polisi na KMKM, wameendelea na zoezi la kutafuata miili ya watu walionasa kwenye vyumba vya meli ya MV Spice Islander iliyozama Jumamosi iliyopita Septemba 10, mwaka huu katika kisiwa kidogo cha Nungw mkoa uliopo Kaskazini mwa mjini wa Zanzibar.


Hata hivyo wazamiaji hao, wameendelea kukabiliana na vikwazo vya kuchafuka kwa hali ya bahari kutokana na upepo mkali uliopelekea mawimbi makubwa na kuisukasuka boti ndogo ya akiba iliyokuwa ikitumiwa na wazamiaji hao kutoka na kurudiu katika meli kubwa ya MV Kasa inayomilikiwa na JWTZ.

Mawimbi hayo yamewafanya wataalamu hao kuwa na wakati mgumu katika safari yao ya kuelekea eneo la tukio kwa lengo la kuendelea na zoezi la uzamiaji na utafutaji wa miili ya watu waliosalia katika meli hiyo siku ya tukio.

Ingawa tangu kupatikana kwa miili 197 siku ya kwanza ya kuzama kwa meli hiyo na miili mingine mitano kupatikana huko kwenye eneo la Shimoni Mombasa nchini Kenya na kufanya idadi ya maiti zilizopatikana kufikia 202, hakuna taarifa zingine za kupatikana kwa manusura ama mwili wa mmoja wa watu waliopoteza maisha yao katika ajali hiyo.

Mpaka sasa, hakuna mategemeo ya kupatikana kwa manusura wengine wa ajali hiyo kutokana na ukweli kwamba mtu hawezi kuishi kwa muda mrefu majini pasipo vifaa maalumu vya kuogelea pamoja na chakula cha kumuongezea nguvu.

Wakati zoezi la kuifikia meli hiyo likiendelea ili kuopoa miili zaidi iliyosalia kwenye vyumba vya meli hiyo, upo uwezekano mkubwa kuwa maiti zitakazopatikana kwenye mabaki ya meli hiyo zitashindwa kutambulika kutokana na kuharibika kwa kuishi muda mrefu majini.

Alipotembelea eneo jirani ilipotokea ajali hiyo kuwapa wananchi pole, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete, alimuagiza Mtaalamu Mshauri wa Maabala ya Jeshi la Polisi nchini Dk. Ahmad Makata, kutumia sayansi ya vinasaba katika utambuzi wa miili ya watu iliyoharibika kiasi cha kutotambulika.

Rais Kikwete alisema kwa kutumia sayansi hiyo, kutawawezesha ndugu na jamaa wa marehemu aliyezikwa na Serikali pasipo kutambuliwa, kuja kutambuliwa siku za usoni baada ya kuwachukua sampuli ya vinasaba watu wanao mtafuta ndugu yao na kulinganisha na vinasaba vya marehemu

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.