
Muwaza imesikitishwa na ajali ya meli ya Spice Islander iliyokuwa safarini kuelekea Pemba. Ajali hio ilitokea alfajiri ya leo tarehe 10.09.2011 sehemu za bahari karibu ya Nungwi kaskazini ya Unguja.
Muwaza inawaombea wale waliopoteza roho zao: kauli thabit, waondoshewe adabu, wasamehewe makosa yao, wapokewe kama mashahidi na walazwe peponi amiin!!
Muwaza inatowa mkono wa rambi rambi kwa jamaa, wema na marafiki wa wafiwa na kuwaombea subra.
inna lillahi wa inna ilaihi rajiuun
Muwaza inaiomba serikali ianzishe uchunguzi wa haraka na wa kina ili kujua kiini cha sababu ili kuepuka ajali kama hizo siku za mbele na kuwachukulia hatua za kisheria wale waliosababisha ajali hio
Dr. Yussuf S. Salim
Mwenyekiti wa Muwaza
No comments:
Post a Comment