Habari za Punde

KUTOKA BARAZANI -SERIKALI YAJIANDAA KUJENGA NYUMBA KWA MAKAAZI YA WANANCHI

Na Mwantanga Ame

WIZARA ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati, inajiandaa kutafuta wawekezaji kwa ajili ya kujenga nyumba kwa makaazi ya Wafanyakazi wa serikali.

Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Haji Mwadini Makame alitoa kauli hiyo barazani jana wakati akijibu suali la Mwakilishi wa Wanawake, Shadya Mohammed Suleiman alietaka kujua endapo serikali ina mpango wa kuzifanyia ukarabati nyumba za serikali za Tibirinzi ziliopo Chake chake Pemba.


Naibu Waziri huyo, alisema serikali sasa inaungalia mpango huo kwa kujenga nyumba zitazokuwa katika hali tofauti ambapo baadhi yake zitakuwa za hali ya juu na hali ya kati na za bei ya chini.

Hatua hiyo ya serikali alisema inalenga kupunguza tatizo la makaazi kwa wananchi wa Zanzibar kwa kuziangalia shida za wananchi katika hali zote.

Akijibu hoja ya nyumba za Tibirizi, alisema serikali inaendelea kuwashajiisha wananchi wanaopewa nyumba za serikali kuzifanyia matengenezo madogo madogo huku Wizara ikiliangalia utekelezaji wa sera yake ya kuwauzia ama kubaki na nyumba hizo.

Aidha alkizungumzia suala la nyongeza la Mwakilishi wa Kiwani, Hija Hassan Hija alietaka kujua kwanini serikali imekuwa ikitowa nyumba za serikali kwa upendeleo na kwanini serikali isifikirie kuwapatia wafanyakazi nyumba za Michenzani.

Naibu Waziri, alisema taarifa hizo hazina ukweli kwani nyumba hizo zimegaiwa kwa watu waliohusika na kupewa watu ambao wanahitaji makaazi na sio kweli kama wizara hiyo imezitoa kwa upendeleo.

Hata hivyo, Naibu huyo alisema serikali imetiliana saini na baadhi ya wawekezaji kwa jili ya kujenga nyumba ambazo baadae watapewa wananchi.

Mwakilishi wa Mtambwe, Salim Hamad Salim alihoji uhalali wa serikali kushindwa kuwapa nyumba watu wanaoendelea kukaa katika nyumba za serikali walizokaa nazo muda mrefu.

Katika jibu lake, Naibu Waziri alisema Wizara yake bado inatekeleza sera ya kuwapatia makaazi wananchi waliokaa kwenye nyumnba za serikali kwa muda mrefu.

1 comment:

  1. Jamani tuweni wakweli, serekali yetu haina tena uwezo wa kuwajengea watu nyumba,si wafanyakazi,si wazee wala raia wa kawaida.'yaliyopita yameshapita sasa hivi hali ya uchumi ni ngumu!'Wawakilishi,zungumzieni mambo yanayowezekana msiulize maswali ilimradi tuu mmeuliza! Lamsingi pimeni viwanja,wawezesheni wafanyakazi wajijengee vibanda vyao! Kwanza wazanzibari wengi hawapendi kuishi nyumba za kupanga kutokana na kuwa na watoto wengi.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.