Habari za Punde

KUTOKA VIWANJA VYA BARAZA WAWAKILISHI CHUKWANI ZANZIBAR.

 WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi wakitoka katika Mjengo wa Baraza baada ya kumaliza Kikao cha Asubuhi cha maswali na Majibu.
 WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mohammed Aboud na Mwakilishi wa Mpendae Mohammed Salum Ndimwa, wakibadilishana mawazo nje ya ukumbi wa mkutano.  
 MWANASHERIA Mkuu wa Serikali Othman Masoud na Mwakilishi wa Mji Mkongwe Jussa Ismail wakijadili jambo nje ya Ukumbi wa Baraza baada ya Kumaliza Kikao cha asubuhi cha maswali na majibu na kupitisha  Mswada.  
WAZIRI wa Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar Nassor Mazrui, akipongezwa na Maofisa wa Wizara yake baada ya kupitishwa kwa Mswada wa Shiruika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC)baada ya kumalizika kikao cha asubuhi.

2 comments:

  1. Jamani nilishtuka kidogo kusikia kuna mswaada wa kuanzishawa kwa shirika la biashara la taifa(ZSTC) wakati najua lipo na linafanya kazi tokea miaka ya 60's.Hivi lilikua halipo pale kisheria au ni mimi tuu sikuelewa vizuri taarifa ile?

    ReplyDelete
  2. Yakhe soma vizuri. Hapakuandikwa mswaada wa kuanzishwa kwa ZSTC.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.