"Kama ndio kwanza unafungulia redio yako, hiki ni kipindi cha salamu kutoka Sauti ya Tanzania Zanzibar.
Nakamata kadi yako ya salamu Bingwa Babu Ally Fuko wa Mlandege dukani, zako salamu ziwafikie ziwapo hazipo wa Kilindi, Msomi Mchanga Issa wa wawi, Bi mize Omar Ally wa Taifu, Wete Pemba, Pucho Khere na Kheri Pucho wa safarini Italy, Simai kahama kwao Kajengwa Makunduchi, Mapengo si Upevu Salum Songoro wa Donge Mdodoni, Abedi Manya na Robo wa Kivunge, Ali Hamza Yahya wa Mtambuuni Mafya, Babi Kisororo wa Kijangwa Mtende na mwisho ni Kombo Mwinyi Shehe wa Sizini Tumbe.
Ujumbe salamu ni nusu ya kuonana. Nazisindikiza salamu zako kwa wimbo wa Abdallah Issa unaitwa JIZIMUE.
hahahah wache mapara,hapo inauma sanaa,kwani kipindi hicho kilukuwa ndio sabu yangu ya roho wakiti nipo nyumbani,ila sasa kila kitu kimekwenda ...
ReplyDeletewow ... hapo ndipo kaka mapara!mbona unaumiza wewe!miaka ile ndio ilikuwa nguja ni njema atakae aje!! leo imekuwa balaa tupu,yaani hasa awepo studioni seleman juma kimea jioni njema hapo raha ndani ya roho..
ReplyDeletebila ya kumsahau ..rafiki yangu ..
Unanikumbusha siku zile niko Pemba nikawa kila siku nasikia Msomi Mchanga Issa wa Wawi ikabidi nikamtafute mpaka nikamuona. Alikuwa maarufu sana huyo mama.
ReplyDeleteMimi walikuwa wakinimaliza hawa waliokuwa safarini Ulaya mara Italy mara Denmark MMhhh nyaani we acha tu
ReplyDeleteKaka mmewasahau wakina Si mzito mzuzu wa potoa na madaraka kigwandu wa Binga-Kisiju..Wakhti mapita wallah! wakati ule nipo 'viko' sec. school hata 1000 yangu mwenyewe similiki!
ReplyDelete