Wamiliki wa Mashamba ya Karafuu, wanaiomba Serikali kupitia Shirika la Biashara la Taifa (ZSTC) , kuwakopesha Fedha ama Vifaa ambavyo vitawasaidia katika zoezi zima la uchumaji wa Karafuu kutokana na Vifaa vingi kuuzwa na watu Binafsi .
Walisema kuwa kuwepo kwa Wafanyabiashara wa Vifaa hivyo binafsi kumewapa matumaini kwamba vifaa vipo kwa wingi, lakini vimekuwa na matatizo katika upatikanaji wake kwa vile wanaviuza kwa fedha Taslim jambo ambalo linapelekea kushindwa kuvimudu.
Hayo waliyaeleza kwa nyakati tafauti wakati Waandishi wa Habari , walipo kuwa na ziara ya kutembelea Makambi ya Karafuu, kuangalia harakati za Uchumaji wa Zao hilo huko Daya , Kisiwani kwa Bint Abeid, Bwagamoyo katika Jimbo la Mtambwe na Pandani Kisiwani Pemba.
Walieleza pamoja na tatizo hilo la Vifaa lakini zoezi la Uchumaji linakwenda Vizuri hasa kwa vile Jua linatoka vizuri pamoja na mvua ndogo ndogo lakini hazijaathiri zoezi hilo.
Mmiliki mmoja wa Zao hilo ambae ana Kambi yake katika Skuli ya Pandani Pemba, Hamad Said Batawi, alimueleza Mwandishi wa Habari hizi kuwa anaiomba Serikali kumkopesha Fedha kiasi cha Tshs, Milion Saba (7,000,000/=) ili aweze kuimarisha Kambi yake hiyo na kuweza kuchuma kwa wingi zao hilo.
Alieleza kuwa kwa sasa anachuma lakini sio vile anavyo tegemea kwani Karafuu anazo za kutosha ingawaje hazija iva kwa pamoja lakini Vifaa vya kutumia katika zoezi hilo bado ni hafifu.
“Mimi nina shida kwa Serikali ,inikopeshe Shilingi million saba , nikizipata hizo basi kambi yangu itakuwa imara na nitachuma Karafuu kwa wingi kwani bado nina tatizo “ alisema .
Kuhusiana na suala la Wachumaji wa Zao hilo Wamiliki hao walieleza kuwa wanaridhika na Bei ya Tshs, 2000/= kwa Pishi moja kwa sasa ambayo wanawalipa wachumaji hao.
Aidha Mkuu wa Manunuzi wa Zao hilo kwa Wilaya ya Wete na Micheweni Pemba, Moh’d Idd Hamad , aliwaeleza Wandishi hao kwamba Shughuli za Ununuzi wa Zao hilo kwa Msimu huu zinakwenda Vyema ukilinganisha na Msimu uliopita kwa Vile Bei ya Ununuzi ni kubwa .
Alisema kuwa kwa siku katika Vituo vyake vya Wete na Micheweni hununuwa Kilo 11,000. ambapo kwa msimu uliopita waliweza kununuwa Tani 25,000 tu kwa Mkoa mzima wa Kaskazini Pemba.
Hivyo aliwapongeza Wananchi walio na Karafuu kutokana na kuwa hadi sasa wanauza katika Shirika la ZSTC, zaidi kuliko mahala pengine hiyo inatokana na Bei ya Karafuu zilivyo kutoka Tshs, 3, 500/= kwa msimu uliopita hadi Tshs, 15,000/= Msimu huu.
No comments:
Post a Comment