SERIKALI ya Zanzibar imewapatia mafunzo vijana 30 wa Unguja na Pemba katika kusimamia miradi ya maendeleo ikiwa ni hatua ya kuwaweka katika mazingira bora ya kutekeleza majukumu ya jumuiya wanazoziongoza.
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Katiba na Sheria Abubakar Khamis Bakary, aliyasema hayo barazani jana alipokuwa akijibu suali la Mwakilishi wa Amani, Fatma Mbarouk Said, aliyetaka kujua kama serikali inampango wa kuwasaidia vijana kuwapa taaluma ya uongozi katika miradi inayoanzisha.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Ustawi wa Jamii Maendeleo ya Wanawake na Watoto, Zainab Mohammed, Waziri huyo alisema serikali imekuwa ikitoa mafunzo hayo.
Alisema mwaka 2009 jumla ya vijana 30 walipatiwa mafunzo hayo kwa kuzingatia umuhimu wa taasisi hizo za kiraia lazima ziweze kutekeleza vyema majukumu yake.
Alisema suala la mafunzo ya uongozi kwa vijana ni moja ya jambo la msingi kwa vile Zanzibar hivi sasa imekuwa na vikundi vingi vya vijana vinavyohitaji kupewa elimu.
Hata hivyo Waziri huyo alisema tatizo kubwa kattika kutekeleza hilo likuja pale Wizara hiyo imekuwa inakosa fedha za kutosha katika kuendesha mafunzo hayo.
Waziri alisema ipo haja kwa vikundi vya kiraia kutumia vyema mafunzo yanayotolewa na taasisi mbali mbali za kiraia ziliopo nchini.
Waziri huyo aliahidi kuendeleza kutoa msaada kwa watendaji wa jumuiya hizo kwa kuwapatia mafunzo mbali mbali kila pale ambapo serikali itapata fursa ya kufanya hivyo.
No comments:
Post a Comment