WANANCHI wa Mji wa ChakeChake wakitafuta mapambo kwa ajili ya watoto wao ili kusherehekea sikukuu ya Eid Al Hajj kesho.
MAANDALIZI ya sikukuu ya Eid Al Hajj kwa Wananchi wa Kisiwani Pemba yapamba katika mitaa mbalimbali kisiwani Pemba kwa kutafuta mahitaji ya Watoto ili waweze kusherehekea Vizuri, kama wanavyoonekana baadhi ya wananchi wakinunua nguo katika mitaa kilima Tindi Chake.
HARAKATI za maandalizi ya Sikukuu katika mitaa ya Mji wa Chakechake yapamba moto kwa pilika pilika za hapa na pale kama wanavyooneka Wananchi picha wakiwa katuika harakati hizo
HARAKATI katika soko jipya la Chakechake Pemba ambalo wananchi wa Chake wamelipa jina la Qutar wakiwa katika harakati za kujipatia mahitaji yao sokoni hapo na kujipatia bidhaa bila ya bughudha yoyote, tafauti na hapo nyuma walipokuwa wakisongana na magari ya abiria yakifika kushusha abiria eneo la sokju kuu la Chake lilikuwa likitowa huduma ya biashara na gari za abiria.
No comments:
Post a Comment