Habari za Punde

LIGI KUU YA ZANZIBAR YATIMUA VUMBI, KATI YA MIEMBENI UNITED 4 VS MIEMBENI 2






 Bendera ya timu ya Miembeni ikipepea Uwanjani wakati timu yao ikiwa imelala kwa mabao 4-2
 MFADHILI wa timu ya Miembeni United Amani Makungu akiwa na Viongozi wa Miembeni asili, katika jukwaa la rushia wakati wa mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar Miembeni United na Miembeni timu ya Miembeni United imeshinda 4-2.


Kocha wa Timu ya Miembeni Rashid Lato akitowa maelekezo kwa timu yake wakati wa mapumziko  

 Mshabiki wa timu ya Miembeni United Mjomba Tomas akivuatilia mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar uliofanyika Uwanja wa Mao.
 Hivi ndivyo ilivyokuwa mchezo wa watani wawili Miembeni United na Miembeni Asili, mchezo uliofanyika uwanja wa Mao timu ya Miembeni United imeshinda 4-2.
Kocha wa timu ya Miembeni Rashid Lato akishangilia timu yake baada ya kupata bao la pili, na kuwakejeli watani wao Miembeni United.  

 Muamuzi wa mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar Kisaka ilibidi apoze koo kwa maji kutokana na mchezo wa watani wawili kati ya Miembeni United na Miembeni, ukiendelea na yeye akipata huduma hiyo kutokana na kazi ngumu uwanjani.  
 Viongozi wa timu ya Miembeni wakiwa hawaamini macho yao kwa matokea ya mchezo wao na Timu ya Miembeni United kwa kuchapwa mabao 4-2.
Wachezaji wa Timu ya Miembeni wakitoka Uwanja baada ya kumalizika kwa mechi yao na Miembeni  mchezo uliofanyika uwanja wa Mao.Miembeni United imeshinda 4-2. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.