Habari za Punde

SAKATA LA MALINDI- YATUPWA TENA CHINI

Na Mwajuma Juma, Zanzibar

CHAMA cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA), jana imetangaza kuishusha daraja la pili timu ya malindi kutokana na kupeleka masuala la soka mahakamani na kuisimamisha Ligi Kuu.

Kwa mujibu wa Msemaji wa chama hicho, Hafidh Ali Twahir alisema barua ya kuishusha Malindi ilipelekwa uongozi wa klabu hiyo juzi, ikiitarifu kwamba mwakani itacheza Ligi Daraja la Pili Wilaya ya Mjini.


Alisema baada ya vikao vilivyofanyika Novemba 2 na 3, timu hiyo ilikubaliwa kucheza Ligi Kuu kwa sharti la kutekeleza taratibu ambazo zitaiwezesha kushiriki ligi hiyo, sharti ambalo pia lilitolewa na Mahakama ya Mkoa ya Zanzibar.

“Tafadhali husika na waraka wa mahakama wa Novemba 4, mwaka huu na pia barua ya ZFA Taifa ya Novemba 5 yenye namba ZFA/MAL/VOL.VII/182 ambayo inajieleza kwa uwazi, kifungu namba 2 cha waraka wa mahakama inakuagiza kutekeleza taratibu zinazohusika ili kubakia Ligu Kuu, ” ilisomeka sehemu ya barua hiyo.

Hata hivyo barua hiyo ilieleza kuwa kutokana na maelekezo hayo ZFA iliwapelekea barua ya kutaka kutekeleza taratibu hizo na kupewa muda wa wiki moja, ambazo imeshindwa kutekeleza.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.