Habari za Punde

SEA GULL, SERENGETI KUTOKA VIFUNGONI?

Zafanyiwa ukaguzi leo

Na Hafsa Golo

KAMPUNI ya Unified Marine Consultant & Services ltd (UMCS), inatarajiwa kuzifanyia ukaguzi meli za Mv. Sea Gull na Mv. Serengeni ambazo zimefungiwa kutoa huduma ya usafiri.

Meli hizo zimefungiwa kwa wakati tofauti baada ya kubainika kuwa na kasoro zinazofanana ambazo zinaweza kuleta janga la usafiri kwa wananchi.


Kabla ya kufungiwa meli ya Sea Gull ilikuwa ikibeba abiria katia ya Zanzibar, Dar es Salaam na Pemba, huku ile ya Seengeti ikisafiri baina ya Unguja na Pemba.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri Vyombo vya bahari, Juma Seif alisema wataalamu wa kampuni hiyo leo, wazifanyia ukaguzi meli hizo.

Alisema ikibainika meli hizo kuwa na kasoro zitaendelea kuzuiliwa kutoa huduma za usafiri kwa wananchi ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.

Alifahamisha kuwa endapo wamiliki wa meli hizo watakuwa wamesharejebisha kasoro zilisababisha kufungiwa, Mamlaka hiyo itaziruhusu ziendelee na majukumu yake ya kawaida.

Akizungumzia sababu ya kuzuiliwa kwa meli hizo, Kaimu huyo alisema ni pamoja na genereta kutokuwepo kwenye maeneo yanayopaswa.

Alisema tatizo jengine lililosababisha kufungiwa ni pamoja meli hiyo kushindwa kutoa maji katika vyumba cha mashine pamoja na kutowaka kwa taa za tahadhari pale mashine zinapozimika.

Katika hatua nyengine Kaimu huyo alisema kuwa kampuni inayomiliki meli Sea Gull, imeshaleta boti mbili ambazo zitasaidia usafiri wa wananchi.
Hata hivyo alishindwa kuweka bayana vyombo hivyo vitasafiri kwa utaratibu upi, kwani suala la biashara huria

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.