Habari za Punde

WAFANYAKAZI WAELIMISHWE SHERIA YA UTUMISHI WA UMMA

Na Haji Nassor, Pemba

MKUU wa Mkoa wa Kusini, Juma Kassim Tindwa, amesema iwapo wafanyakazi wataifahamu vyema sheria namba 2 ya mwaka 2011 ya Utumishi wa Umma, inaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa, migogoro isiokua ya lazima baina yao na mwajiri.

Tindwa alitoa kauli hiyo jana huko afisini kwake mjini ChakeChake alipokua akizungumza na wajumbe na maofisa wa Tume ya Utumishi serikalini ambayo tume hiyo ipo Kisiwani Pemba kwa ajli ya kuwapa taaluma watendaji wa Serikali, juu ya sheria mpya ya utumishi.


Alisema kuwa kwa vile Tume hiyo imeazimia kuwafahamisha watendaji wakuu wa serikali Kisiwani humo ikiwa ni pamoja na maafisa wadhamini, maofisa tawala Mkoa na wilaya pamoja na watedaji wengine, inaweza kusaidia kwa wafanyakazi kuelewa sheria hiyo.

Alieleza kuwa, kwa vile pia sheria hiyo namba 2 ni mpya miongoni mwa wafanyakazi na watendaji waliowengi itakua ni chachu ya mafanikio kwa tume hiyo itakapo wapa taaluma watendaji wakuu wa Serikali Kisiwani Pemba na kisha wao kuisambaaza kwa wafanyakazi wao.

‘’Kwa vile hata watendaji wakuu wa Seikali hawaifahamu vya kutosha sheria hiyo, pindi wakipatiwa taaluma hiyo itasaidia kwa wafanyakazi kutambua haki zao na wajibu wao wanapokua kazini’’,alifafanmua Tindwa.

Mapema mjumbe wa tume hiyo Yussuf Salim Ali alisema kua asubuhi hii (leo Alhamis) wanatarajia kua na kikao cha pamoja na watendaji ambali mbali wa Wizara zilizopo Pemba, ikiwa ni pamoja na maafisa wadhamini, maafisa tawala mkoa na wilaya ili kuitambua sheria hiyo.

Alisema kua kwa vile kuna sheria mpya namba 2 ya mwaka 2011 ya Utumishi wa Umma ,ambayo ilipitishwa na baraza la wawakilishi hivi karibuni, wafanyakazi na watendaji waliowengi hawaifamu ndio maana wamenzia Kisiwani Pemba kwa kufahamisha.

‘’Sheria hii ni mpya na imepitishwa na baraza la wawakilishi hivi karibuni na sisi wajumbe pamoja na maafisa wa tume hii tumeona ni vyema tukaanzia Pemba ili kuwafahamisha watendaji wakuu ‘’,alieleza Mjumbe huyo.

Nae Katibu wa tume hiyo Khamis Mohamed alisema kua, anaamini mara baada ya kutoa mafunzo hayo leo hii wanatarajia kwa watendaji hao kupata ufanisi wa hali juuu na kuwafahamisha wafanyakazi wao .

Alieleza kua imebainika kwamba wafanyakazi waliowengi hawazifahamu kanuni na sheria zinzaowaongoza wanapokua kazini na kwa baadhi ya wakati kusababisha migogoro hata miongoni mwao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.