Habari za Punde

DK SHEIN AFUNGUA MAONESHO YA MIAKA 50 YA UHURU DAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa mkurugenzi mtendaji katika Afisi ya Rais wa tanzania Ladius J. Mwamanga,alipotembelea maonesho ya bidhaa za chakula katika banda la Afisi hiyo jana,katika mwendelezo wa miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara katika uwanja wa Mwalimu Julius K.Nyerere Jijini Dar es Salaam jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akipata maelezo yaa redio aliyoitumia marehemu mwalimu J.k Nyerere wakati wa uhai wake,kutoka Paulo afisa muhifadi makumbusho ya taifa,wakati wa alipotembela maonesho maonesho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara katika uwanja wa Mwalimu Julius K.Nyerere Jijini Dar es Salaam jana
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akiangalia zana za kilimo na kupata maelezo kutoka kwa Afisa ,katika Wizara ya kilimo Chakula na ushirika Linus A. ngowi,baada ya ufunguzi wa maonesho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara katika uwanja wa Mwalimu Julius K.Nyerere Jijini Dar es Salaam jana.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akibonyeza kitufe kuashiria ufunguzi wa maonesho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara katika uwanja wa Mwalimu Julius K.Nyerere Jijini Dar es Salaam jana.

Picha zote na Ramadhan Othman

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.