Habari za Punde

MBUNGE BUBUBU AWATAKA WANANCHI KUSHIRIKI MABADILIKO YA KATIBA

Na Husna Sheha

MBUNGE wa jimbo la Bububu, Juma Sururu Juma amewahimiza wananchi wa Sharifumsa kushiriki kwa wingi katika kupiga kura maoni kuchangia mabadiliko ya katiba.

Alisema hayo katika tawi la CCM Sharifumsa wakati alipokuwa katika ziara ya kutembelea matawi pamoja na wananchi wa jimbo hilo akiwaelimisha kuhusu kazi itakayowakabili ya kutoa mchango wao kwenye
suala la nmapendekezo ya mabadiliko ya katiba.


Alisema madhumuni ya mabadiliko ya katiba hiyo ni kuweka utaratibu wa kuunda tume itakayokusanya na kuratibu maoni ya wananchi pamoja na kuweka utaratibu utakaoweza kuchambua rasimu ya mswaada wa katiba mpya

Vile vile aliwaeleza kuwa Tume itayokuwa ikikusanya maoni hayo ya wananchi itatoa nafasi kwa kila mwenye maoni yake kuwasilisha lakini akawaonya kujiepusha namakundi yenye muelekeo wa kupinga muungano
suala ambalo linahatari zake.

Pamoja na kueleza kwamba kila mtu atakuwa na jukumu lake la kuwasilisha maoni yake lakini ni vyema wanaCCM wakaellimishwa kujua hasa ni ni wajibu wa wananchi katika mabadiliko hayo.

Aidha, aliwaeleza kuwa wananchi watapata elimu maalum ili kuepuka na kuja kukosea kujibu maswali watakayoulizwa.hivyo amewaomba wanachi hao kuyakubali mabadiliko ya katiba hiyo kwa kuzingatia mambo ya msingi zaidi na sio kuchangia mambo ambayo hayataweza kuwasaidia hapo baadae.

Alisema muda wa sasa ni kipindi kizuri na ni muafaka kwa wananchi kitumia naffasi hiyo kuchangia mambo ya maana na kama hawaelewi wajibu wao basi watawasadia kujua nini hasa ni muhimu kuchangiwa na mengine
kuyaacha.

Hata hivyo, Mbunge huyo amewashauri kinamama kuanzisha vikundi mbali mbali vya ushirika ili kuweza kujiletea maendeleo pamoja na kujikwamua na ukali wa maisha .

Aidha, aliwashauri vijana kutafuta kazi za kujiajiri wenyewe bila kusubiri nafasi za ajira kutoka serikalini kutokana na uchache wa nafasi za aina hiyo.


Pia Mbunge huyo alisema mipango inatayarishwa kutafuta nafasi za ajira kwa kuimarisha makundi ya wanajamii kupatiwa miradi ya kudumu ambayo itawezesha kujiajiri wenyewe.

Kuhusu tatizo la maji, katika jimbo lao mbunge huiyo alisema wananchi wanapaswa kuwa wavumilivu kwa muda huu jitihada zinafanyika kutafuta mashine ya kusukumia maji katika chemchem ya Mwanyanya.

2 comments:

  1. KICHWA CHA HABARI KINASEMA "MBUNGE BUBU......"Makusudio ni mbunge ni mlemavu wa kusema au ni kosa la uandishi?

    ReplyDelete
  2. Kosa la uandishi. Tumelirekebisha na ahsante kwa kutuzindua

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.