WAANDISHI wa habari wametakiwa kuyafikia makundi ya makabila mengine katika kufuatilia vitendo vya ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia badala ya kuwaangalia waafrika pekee kama ndio wanaoathirika na matatizo ya aina hiyo.
Alfred Mbogora, Mkufunzi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), akitoa mada juu ya suala la maadili katika kuripoti habari, kwenye mafunzo yanyoendelea kwa Waandishi wa Habari juu ya Ukatili kwa Watoto inayofanyika katika ukumbi wa Baraza la Habari Mlandege Mjini Zanzibar.
Alfred, alisema imeonekana kwa waandishi wengi wamekuwa wanashindwa kuyafikia makabila mengine katika kufanya nao mahojiano juu ya vitendo vya ubakaji ama unyanyasaji wa kijinsia yanayowahusu watoto jambo ambalo ni la ubaguzi na limekuwa likiijenga jamii kuwa watu wenye asili ya kiafrika ndio pekee wanofanyiwa vitendo hivyo.
Alisema dhana hiyo inahitaji kupigwa vita na waandishi wa habari kwa kuona wanafanya kazi zao kwa kuyaangalia makundi ya kijamii yote bila ya ubaguzi kwani wapo watoto wenye asili nyengine ambao wamekuwa wakipata mateso ndani ya familia zao.
Alisema hiyo inajidhihirisha katika kesi nyingi ambazo wameshawahi kuzipokea kuona ni zile zinazohusiana na nasaba ya kiafrika huku kukiwa ripoti zinazowahusu watu wenye asili ya kiarabu, kiasia na makabila mengine.
Kutokana na hali hiyo Alfred, alisem ni vyema kwa waandishi wa habari kuiona hali hiyo na kuiepuka ili wasiwe katika kundi la kujenga ubaguzi katika jamii kwa kuacha kuwasaidia makundi ya makabila mingine.
Alisema hiyo itasaidia kuona suala la unyanyasaji wa kijinsi sio lenye kuwahusu watu wenye asili ya waafrika pekee bali na hata nasaba nyengine yanayaweza kuwapata.
"Kuna matabaka mengi katika jamii lakini linalohojiwa ni la waswahili watupu kuna matatizo ndani ya familia za waarabu, wahindi wote wanpata unyanyasaji wa hali ya ju lakini tunajenga ni waafrika tuu ndio wanaobakwa" Alisema Alfred.
Akiendelea mkufunzi huyo pia alikemea kwa waandishi wa habari kuona hawafanyi kazi zao kiujanja kwa kushindwa kuwaeleza wazi watu wanaofanya nao kazi katika shughuli zao.
Mapema Mtoa mada juu ya Sheria za unyanyasaji wa kijinsia kwa Zanzibar, kutoka afisi ya Wizara ya Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto Mwanasheria wa Afisi hiyo Didas Halfan, alisema bado kuna tatizo katika kusimamia utekelezaji wa sheria za kunajisiwa watoto kunkosababishwa na ufahamu mdogo wa mazingira ya kisheria.
Alisema matatizo ya kubakwa ama kuingiliwa kwa nguvu bado ni jambo linalowaumbua watoto wengi wa zanzibar kutokana na hivi sasa kuonekana utekelezaji wake kuwa mgumu baada ya baadhi ya wanajamii kuwa ni miongoni mwa wanaotenda vitendo hivyo.
Alisema katika utafiti ambao ulifanywa na wizara hiyo umebaini kuwepo kwa watoto walioathirika wakiwa katika vyuo vya madrasa na wengine maskulini na katika familia zao.
Alisema kutokana na hali hiyo ipo haja ya kuona waandishi wa habari nao wanashiriki kuisoma vyema sheria mpya ya kuwalinda watoto na kuielimisha jamii ili iweze kuifanya jamii kuitambua na kuyaelewa maeneo ambayo wataweza kuyatumia kutatua matatizo ya aina hiyo yatapowakumba.
Hata hivyo Mwanasheria huyo alisema katika jitihada za Wizara hiyo imeanza kujiandaa kwa kuanzisha mtandao utaoiwezesha jamii kuutumia kwa ajili ya kutoa taarifa za ubakaji pindi zitapowakuta hata wakiw mbali ya vituo vya Polisi hatua ambayo itasaidia kupatikana kwa wahalifu kwa haraka.
No comments:
Post a Comment