Habari za Punde

ZANZIBAR IJIDHATITI UTALII WA NDANI

Na Ramadhan Makame, China

WAZIRI wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui, amesema umefika wakati Zanzibar kuacha kuutegemea sana utalii wa nje ambao uhakika wake ni mdogo hasa katika kipindi hichi cha mgogoro wa kifedha.

Waziri huyo alieleza hayo baada ya kuteremka katika ukuta wa Great Wall, ambapo jana viongozi wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar walipata fursa ya kuupanda ukuta huo uliojengwa karne ya saba.


Alisema suala la kutegemea utalii wa nje hasa kwa nchi za Ulaya linaweza kuyumbisha uchumi wa Zanzibar, kwani hivi sasa nchi nyingi za bara hilo zimekuwa zikikabliwa na mdororo wa fedha na uchumi huku baadhi ya serikali za bara hilo zikikaribia kufilisika.

Alisema ili kuepukana na tatizo hilo ni muhimu sekta ya utalii ikaangaliwa upya huku msisitizo ukiwa ushajiishaji wa utalii wa ndani kama nchi za Asia zinavyofanya ikiwemo China.

"Umefika wakati Zanzibar kuviimarisha vivutio vyake vya utalii na kuhamasisha utalii wa ndani kama wenzetu wa China walivyouimarisha utalii wao", alisema waziri huyo.

Aidha alisema vivutio vya utalii Zanzibar vipo ila havijafanyiwa kazi ipasavyo katika kuimarishwa na wananchi kushajiisha ikiwa ni pamoja na Ngomekongwe, People Palace, Beit al Jaib na vyenginevyo.

Mazrui alifahamisha kuwa Zanzibar kuwa iko Tanzania, eneo la Afrika Mashariki pamoja na maeneo mengine ya kikanda ni muhimu kiutalii lakini lazima watu washajiishwe.

"Hatujafanya vizuri sana katika utalii wa ndani kama walivyofanya wenzetu wa China, nadhani umefika wakati tubadilike hasa kutoka na hali ya uchumi wa dunia unavyokwenda.

Kwa upande wake Mwakilishi wa kuteuliwa, Asha Bakari Makame, alisema Zanzibar inakabiliwa na matatizo sugu katika sekta ya utalii hasa ikiwemo tatizo la uvujaji wa mapato.

"Tumejifunza kwa wenzetu hapa China wako makini hakuna nafasi ya kuchakachua fedha kwenye utalii, iwe wa ndani au hata ule wa nje, tatizo letu ni udokozi ambao ndio unaotusumbua", alisema.

Aidha alifahamisha kuwa ni jambo la kushangaza kwamba hivi sasa Zanzibar haielewi watalii wanaoingia nchini hali inayotilia mashaka uwepo wa uvujaji wa mapato.

Mwakilishi huyo pia alisema pia Zanzibar imekuwa haiko makini kwani wawekezaji waliokaribishwa wengi wao walikuwa matapeli hali inayosababisha kukwepa ushuru na wengine kukimbia.

Naye Mkuu wa kitengo cha ushirikiano kutoka wizara Nchi Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo, Ramadhan Khamis Juma alisema mabadiliko yanahitajika katka visiwa vya Zanzibar kama kweli inataka kukuza utalii.

"Hatujawa makini sana katika kukuza utalii wetu, tukilinganisha na wenzetu hapa China, wao wana mipango, wanatunza vivutio vyao na wanajua nini wanachokifanya", alisema ofisa huyo.

Viongozi hao jana walipata fursa ya kutembelea na kupada Great Wall ambao wachache walifika kileleni hasa kutokana na hali mbaya ya hewailiyoko kwenye eneo hilo wakati huu.

Mbali ya eneo hilo pia walitembelea kijiji cha Olimpiki, kiwanja cha kilichofanyika michuano ya Olimpiki ya mwaka 2008 pamoja na maeneo mbali mbali ya vivutio vya utalii.

2 comments:

  1. UTALII WA NDANI NI KAMA HIVI,
    KWA WALE AMBAO WANAISHI NCHI ZA ULAYA WANAWEZA KUJIONEA JINSI WATU WANAVYOFANYA VIZURI KATIKA NYANJA MABLIMBALI,UKIANGALIA KAMA KULE TURKEY KATIKA MJI WA ISTANBUL UTAPATA USAFIRI SIO TU WA BARABARANI AU CHINI YA ARDI,BALI KUNA BOTI ZA KISASA AMBAZO HUWA NI VIUNGANISHI MUHIMU SANA KWA WANANCHI NA NJIA YA MKATO KWA WASAFIRI NA PIA KUIINGIZIA NCHI FEDHA JINGI PAMOJA NA WANANCHI KUFANYA SHUGHULI ZAO KWA UFANISI ZAIDI NA MPANGO ULE NI BORA KWA HAPO NYMBANI, ZILE BOTI ZINAKUWA ZINATEMBEA KUPITI KATIKA FUKWE ZA MIJI YAO YOTE,KWAMFANO BOTI IKITOKEA MALINDI AU FORODHANI -INAUNGANISHA SAFARI BUBUBU KWA NJIA YA MAJI NA NYINGINE INATEMBEA KWENDA MJI MWINGINE KUUNGANISHA TUMBATU NA SEHEMU YA KARIBU YAKE,AMBAPO KILA BAADA YA DAKIKA AU SAA KUNAKUWA TAYARI BOTI INAKUJA NA BOTI INAONDOKA KWAMFANO KUTOKA FORODHANI KUELEKEA PRISONER ISLAND-AMBAPO KULE BOTI NYINGINE INAELEKEA BUBUBU NA YA INAKWENDA PRISONER ISLAND NA KUFIKIA FORODHANI KWA MZUNGUKO WA KAKISIWA CHETU CHOTE CHA UNGUJA NA PEMBA NA KULE NUNGWI KUNA FERI BOTI KUBWA AMBAYO KAZI YAKE NI YA KUUNGANISHA KUTOKA NUNGWI HADI MWANZO WA NCHA YA KISIWA CHA PEMBA AMBAPO KUWE NA UTARATIBU BOTI MOJA ILIENDA PEMBA MOJA YA PEMBA INAKUJA UNGUJA,HADI KUFIKIA BOTI MBILI AU TATU ZIKIWA ZINAPISHA KWENDA UGUNJ/NA PEMBA SIKU ZA BAADA ILI KUTOA NAFASI YA MTU KWENDA KATIKA WISIWA HIVYO SIKU HIO HIO NA KUREJEA SIKU HIO HIO PALE ATAKAPOTAKA TU,AMBAPO ITATOA FURSA KWA WAKULIMA WA NCHI HIZO KUWEZA KUVUUKA NA WAZAO YAO KWENDA KUUZA SEHEMU NYINGINE KIURAHISI KULIKO UTARATIBU WA ZAMANI WA KUSAFIRI KUTOKA MALINDI HADI MKOANI AU WETE PEMBA USAFIRI WA SIKU NZIMA WAKATI HIVI SASA WATU WAKO KTK KUZIUNGANISHA NCHI KWA MADARAJA MAKUBWA SISI TUNAHITAJIA FERRY BOTI KUBWA ZA KUZIUNGANISHA NA KUTOA USAFIRI WA KILEO NA SIO KAMA ULIVYOZOELEKA TOKEA DUNIA INAUBWA HADI LEO KUTOKA MALINDI MPAKA MKOANI BADALA YA POINT YA MWISHO YA RAS YA UNGUJA NA POINT YA MWISHO YA RAS YA PEMBA NA HIVYO HIVYO KUTOKA UNGUJA KWENDA BARA BOTI KUZIUNGANISHA RAS NA RAS YA KULE BARA NA UPANDE WA WETE KUUNGANISHE ILE RAS YA MWISHO WATU WALIYOKUWA WAKISEMA ILIKUWA NI HARAMU KUPITISHIA MAGENDEO KWENYA IFUNGULIWE IWE HALALI ILI BINADAMU KULE WAENDE KUNUNUA NA KUUZA KIHALALI NA PIA KUIPATIA SERIKALI MANUFAA KWA MALIPO YA ADA ZA BIDHAA HIZO PIA KUWAFANYA WATU KUTEMBELEANA KWA NJIA RAHISI ZAIDI,KUTOKANA NA MPANGO HUO TUTAJIKUTA WAZANZIBAR WOTE WATAKUWA NI WATALII KWANI KUTAKUWA NA VYOMBO VYA KUWAUNGANISHA MARA KWA MARA NA VYA UHAKIKA MTU KUREJEA NYUMBANI WAKATI WOWTE ANAOTAKA,
    AHSANTE.

    ReplyDelete
  2. summarize shekhe vipi bwana waandika kama waongeeeaa!!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.