Na Mwandishi maalum, Davos
WAZIRI Mkuu wa Uingereza, David Cameron ameipongeza Tanzania kuwa mfano wa kuigwa katika kuleta mabadiliko chanya kwenye ekta za kilimo na elimu barani Afrika.
Waziri huyo alitoa pongezi hizo alipokuwa akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete huko mjini Davos nchini Switzerland, ambapo viongozi hao wanahudhuria mkutano wa World Economic Forum (WEF).
Cameron alimueleza Rais Kikwete kuwa Tanzania ni nchi inayosatahiki kuigwa kutokana na mabadiliko ya kilimo hasa kwenye wakati huu.
“Afrika inapitia kipindi cha mabadiliko ambayo ni chanya, na Tanzania ni mfano bora wa kuigwa katika hili”, alisema Cameron alimueleza Rais Kikwete.
Kwa upande wake Rais Kikwete alimueleza waziri huyo kuwa Cameron kuwa kilimo ni sekta kubwa na inayotegemewa na Watanzania wengi na kwamba serikali inalenga katika kukuza kilimo kwa ajili ya kujitosheleza kwa chakula.
Mapema jana asubuhi, Rais Kikwete alijumuika na viongozi wengine kutoka Ethiopia, Guinea-Conackry, Kenya na Afrika Kusini kuzungumzia mabadiliko mbalimbali ya uchumi na maendeleo barani Afrika.
Katika mjadala huo uliongozwa na waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Gordon Brown, ambapo Rais Kikwete alisema pamoja na mabadiliko hayo, bara la Afrika nalo ni sehemu ya dunia uchumi, hivyo nayo kupata athari mbalimbali zinazotokana na mabadiliko hayo ya kiuchumi duniani.
Rais alisema pamoja na athari na mabadiliko ya kiuchumi duniani, bado Afrika ina mahitaji zaidi katika kutekeleza sera zinazolenga katika uchumi imara na kuwekeza zaidi katika sekta za elimu, utafiti, kilimo,
viwanda na miundombinu.
Rais Kikwete pia amefanya mazungumzo na viongozi na wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo Bill Gates, pamoja na viongozi wa Ethiopia na Kenya ambapo wamezungumzia namna ambayo Gates atatoa mchango wake zaidi katika masuala ya kilimo na utafiti.
Aidha Rais Kikwete alikutana na kufanya mazungumzo na Sadako Ogata, Rais wa Shirika la Misaada la Japan, (JICA) ambaye alisema shirika hilo litaendelea kutoa misaada mbalimbali kwa Tanzania pamoja na
kwamba yeye amefikia kipindi chakustaafu.
Rais Kikwete pia amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodafone, Vittorio Colao ambaye ameonesha nia ya kusaidia Tanzania katika kutoa na kusambaza elimu kwa kutumia simu za mkononi
katika masuala mbalimbali ya afya, kilimo na elimu.
No comments:
Post a Comment