Habari za Punde

Jamii Iache Tabia ya Kuwanyanyapaa Wenye VVU

Na John Mpiga Picha

OFISA programu kutoka Jumuia ya watu waishio na virusi vya UKIMWI ZAPHA+ Zanzibar, Masoud Nassor amesema watu wanaoishi na virusi vya maradhi hayo wamekuwa wakikabiliwa na changamoto kubwa ya unyanyapaa.

Alisema kuwa watu wenye kuishi na virusi hivyo wamekuwa akipatwa na tatizo hilo kwa njia mbali mbali katika jamii ikiwemo kusimangwa pamoja na kufanyiwa utani kutokana na hali yao.


Ofisa huyo alieleza hayo hivi karibuni huko Mgambo wilaya ya Kaskazini ‘B’, na kuwasihi wananchi wa kijiji hicho kuacha kufanya kuwafanyia unyanyapaa na kuishi nao kwa wema kwani ni watu wenye kuishi na virusi
ni wanadamu na wanahitaji haki zao kama watu wengine.

Alisema endapo jamii itaendelea utamaduni wa kuwanyanyapaa watu wenye kuishi na VVU, tatizo la UKIMWI litakuwa gumu kumalizika katika jamii.

Masoud alisema kutokana na mantiki hiyo unyanyapaa na ubaguzi kwa wanaoishi na virusi vya UKIMWI hawakubaliki kwani tatizo hilo halitapunguza tatizo hilo lenye kuikabili jamii.

Aidha alifahamisha kuwa kama hali hiyo haitomalizika basi hisia za maumivu ya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI kutokana na unyanyapaa na ubaguzi katika ngazi ya jamii ni mbaya na huo pia upo katika majina
yanayoitwa katika hali ambayo si ya kawaida.

Akielezea mikakati ya ZAPHA+, alisema jumuia hiyo itaendelea kuielimisha jamii juu ya madhara yanayosababishwa na janga la UKIMWI pamoja na kuitaka jamii kubadilika ili kupunguza kasi ya maambukizi mapya

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.