Habari za Punde

Dk Karume Azindua Skuli ya Mwembeshauri Kuadhimisha Miaka 48 ya Mapinduzi

Rais Mstaafu wa awamu ya sita Zanzibar Dk.Aman Karume akihutubia wananchi walimu na wanafunzi waliohudhuria katika uzinduzi wa Jengo la Ghorofa moja la Skuli ya Mwembe shauri, kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi na mwengine ni Mke wa Rais huyo mstaafu Mama Shadya Karume ikiwa ni shamra shamra za kutimia miaka 48 ya Mapinduzi


Rais Mstaafu wa awamu ya sita Zanzibar Dk.Aman Karume akisalimiana na wanafunzi wa Skuli ya Mwembe shauri kabla ya kuzindua jengo la Ghorofa moja la Skuli hiyo, kulia kwake ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ramadhan Abdulla Shaabani ikiwa ni shamra shamra za kutimia miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar
Rais Mstaafu wa awamu ya sita Zanzibar Dk.Aman Karume akipatiwa maelezo na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ramadhan Abdulla Shaabani kuhusu moja ya madarasa ya Skuli hiyo ya Ghorofa moja iliyojengwa Mwembe shauri Zanzibar ikiwa ni shamra shamra za kutimia miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar
Rais Mstaafu wa awamu ya sita Zanzibar Dk.Aman Karume akifunguwa kitambaa kuashiria uzinduzi wa jengo jipya la ghorofa moja la Skuli ya Mwembe shauri ikiwa ni shamra shamra za kutimia miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Rais Mstaafu wa awamu ya sita Zanzibar Dk.Aman Karume akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo jipya la ghorofa moja la Skuli ya Mwembe shauri ikiwa ni shamra shamra za kutimia miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Picha zote na Yussuf Simai Maelezo

1 comment:

  1. Ni hatuwa ya kimaendeleo na inatia moyo lakini nna wasiwasi ya hali ya jengo baada ya kuona hiyo sakafu ilivyo chafu humo ndani wakati hili jengo ni jipya au ni katika kuharakisha ufunguzi?
    Vile vile nimesikitishwa baada a kuona bei ya mabuku yaani shs.1000 kwa buku na yanauzwa kwa dazen yaani 12 kwa pamoja.Iko wapi ELIMU BURE KWELI MNYONGE ATASOMA JAMANI...............

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.