Na Zahira Bilal Maelezo
Waziri wa kazi uwezeshaji wananchi kiuchumi na ushirika Haroun Ali Suleiman amesema kuwa idadi ya vyama vya ushirika vinavyoaandikishwa imekuwa ikiongezeka na kwamba vyama hivyo vimekuwa vikiongezewa nguvu ya usimamizi na utaalamu.
Hayo aliyasema leo wakati akijibu swala la Mwakilishi wa nafasi za wanawake Salma Mussa Bilali alietaka kujua hatua zinazochukuliwa na wizara katika kuimarisha vyama vya ushirika wilayani huko katika ukumbi wa baraza la wakilishi chukwani
Waziri Haroun alisema kuwa zoezi la kukusanya takwimu za vyama litakapokamilika litasaidia kujua mahitaji ya wataalamu na watendaji kwa ujumla
Aidha alisema wizara yake inajitahidi kujipanga ili kuweza kuimarisha utendaji wilayani na katika vitengo maalumu vya idara ya ushirika pia kusimamia mpango wa mafunzo kwa maofisa wa ushirika wa ngazi mbali mbali ili kuongeza utaalamu na uwezo wao wa kuhudumia vyama vya ushirika kwa ufanisi zaidi
Alisema wizara yake inampango wa kuanzisha vituo vya stadi maalumu kwa ajili ya kutoa elimu kwa washirika na kuweza kuimarisha vyama vya ushirika kwa kila wilaya
Alisema kufanya hivyo inaweza kuondoa usumbufu wa tatizo la ucheleweshaji wa usajili wa vyama vya ushirika na kuongeza kasi ya kukagua na kupewa usajili kwa haraka
Sambamba na hayo alisema kufanya hivyo ni kuwawasaidia wananchi wa mijini na vijijini kupata ajira na kuwaondoshea umasikini na ndio malengo ya wizara hiyo
No comments:
Post a Comment