Habari za Punde

Innaa Lillaahi Wainnaa Ilayhi Raaji'un - 'Jamhuri' Hatunaye tena


Jumuiya ya Watanzania nchini Ugiriki inasikitika kutangaza kifo cha ndugu yetu Haroun Abdallah Othman ambae alikuwa akijulikana zaidi kama Jamhuri kilichotokea Hospitali ya Nikeas Piraeus siku ya Jumamosi 18/02/12.
Kabla ya kuishi Ugiriki Marehemu alikuwa ni mkaazi wa mitaa ya Kikwajuni. Jumuiya ya Watanzania Ugiriki imo katika hatua za kukusanya michango kwa ajili ya kuusafirisha mwili wa Marehemu nyumbani.
Mola amlaze mahala pema peponi. Aamin

Kayu Ligopora
Katibu Mkuu 
Jumuiya ya Watanzania Ugiriki

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.