Habari za Punde

Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi na Bahari Kuu Yazitaka SMT na SMZ Kuridhia Sheria



Na Ali Issa Maelezo

Mamlaka ya kusimamia uvuvi wa bahari kuu Tanzania imeiambia serikali ya jamuhuri ya muungano Tanzania na ile ya Zanzibar kuiridhia sheria ilopo na kuipitisha ili weze kufanya kazi zake vizuri na kutekeleza vyema kazi zake mamlaka.

Hiyo imesemwa leo huko kinazini katika jengo la ZSTC Zanzibar na Mkurugenzi wa mamlaka hiyo Geofrey Frank Nanyaro wakati wa mazungumzo kati ya malaka na Wizara inayo shughulikia masuala ya muungano Tanzania mbele ya waziri Samia Suluhu Hasani aliyefika hapo akiwa ziarani kutembelea maeneo hayo .

Amesema mamlaka ya kusimamia bahari kuu ni taasisi iliyoundwa kupitia sheria ya malaka ya kusimamia uvuvi kwenye eneo la ukanda wa kiuchumi EEZ ya mwaka 1998 ambayo ilifanyiwa marekebisho kupitia sheria namba nne ya mwaka 2009 sheria ambayo ilishirikisha pande zote mbili za muungano na baadaye ikapelekwa baraza la mawaziri na kukubaliwa lakini upande wa pili wa baraza la wawakilishi hadi sasa bado kuridhia sheria hiyo .


Amesema kuchelewa baraza la wawakilishi kuridhia sheria hiyo ni kufanya kazi katika mazingira ambayo hayaendani na kazi kisheria na kuyafanya kuwa mazingira magumu katika utekelezaji wakazi zake kitaalamu .

“Ni vigumu kutekeleza kazi zetu kitaalamu kwani sheria ndiyo inayo muongoza mtu kufanya kazi vyema hivyo ikawa sheria haijaridhiwa itakuwaje juu ya kusimamia bahari kuu ambayo watu wanao kuja kuvua wanafahamu kila kitu .”alisema Geofrey .

Aidha mkurugenzi huyo alisema kuwa kuchelewa kuridhiwa kwa sheria hiyo kuna wakosesha fursa wataalamu wao hata kupata mafao yao kimsingi kama vile mishahara jambo ambalo linapelekea wataalamu hao kupata posho tu.

Amesema hali hiyo haipendezi kwani inaleta uchovu katka uwajibikaji na misingi bora ya kazi .

Nae mtaalamu wa mtambo unao toa ripoti za meli za kigeni zinazo ingia nchini Damian Boniface Chando amesema kuwa Mamlaka hiyo hivi sasa ina uwezo wa kugundua meli zinazoingia na kutoka katika ukanda wa bahari kuu zinazovua samaki kinyemela kwa kutumia mtambo wa Vessl monitoring system ambao wanao na unafanyakazi muda wote.

Aidha alisema kuwa mtambo huo unaweza usifanye kazi iwapo mabaharia watafanya uharamia kwa kuzima kifaa kiitwacho kwa kitaalamu transimitter na wao wasiweze kugundua kama samaki wanavuliwa kwa wizi.

“Nivi zuri kujipanga kua na doria kwani mtambo huu hautoshi peke yake iwapo mabaharia watafanya uharamia na kuzima mitambo yao’alisema Boniface .

Nae waziri Samia alisema wanazichukuwa changamoto zilopo na kwenda kuzifanyiakazi, lakini alisema kua wakati umefika kwa viongozi kuwa wa wazi na wakweli wanapokuwa katika vikao na kutekeleza yale wanayo ya sema

Amesema katika ziara yake amejifunza mengi ambayo alikuwa hayajui na sasa anaelewa na atayapeleka kunako husika na kufanyiwa kazi.

Waziri huyo alitembelea mamlaka ya Uvuvi wa Bahari kuu Fumba, MACEP Bweleo kuangalia madawati yaliyotolewa na TASAF katika skuli ya Kombeni pamoja na mradi wa kinamama wakutengeneza sabuni za kuogea kwa kutumia malighafi ya mwani na pete za luu kwa kutumia malighafi ya kombe za baharini

2 comments:

  1. Ilikuwaje ikaundwa mamlaka hii bila ya kukubaliwa na pande zote mbili?

    ReplyDelete
  2. Hatutaki ondokeni na mitambo yenu Watanganyika,wache wavuliwe samaki mpaka wamalize.Sisi tushachoka na nyinyi wezi wakubwa mipaka na bahari kuu ya Zanzibar haiwahusu wezi wakubwa.Sisi hatutaki muungano na nyinyi tushachoka nanyi wakoloni weusi,huu ni wakati wa Zanzibar kuwa huru na kufanya mambo yake wenyewe.Hamna mnachokitafuta Zanzibar kama si mali zake,washenzi hatutaki muungano na watu wasiokuwa na imani,wanaowauwa walemavu wa ngozi burebure na wazee kwa sababu eti wachawi.
    watanganyika wauwaji na wezi hatutaki hatutaki, hatutaki, na hatusikii lolote mpaka kieleweke.....Muungano mwish Chumbe

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.