Habari za Punde

Serikali Itaendelea Kushirikiana na Wataalamu, Watafiti

Na Raya Hamad (OMKR) 

Katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais inaendelea kushirikiana na wataalamu mbali mbali ili kutaarisha tafiti zinazohusu mabadiliko ya nchi na athari zake kwa uchumi wa Zanzibar .

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dk Islam Seif amesema utafiti huo utasaidia kupata taarifa za awali kwa ajili ya kutayarisha mpango mkakati wakukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi .

Dk Islam ameyasema hayo wakati alipokuwa na kikao cha pamoja kati ya wataalamu wa utafiti kilichofanyika Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais na ujumbe wa wataalam wane unaoongozwa na mshauri mwelekezi Kutoka Umoja wa Mataifa Paul Watkis .

Aidha Dk Islam amewataka wataalamu hao kujali na kuzingatia muda wa makubaliano uliowekwa wa kuwasilisha rasimu mapema iwezekanavyo kwa mujibu wa makubaliano ili hatimae ziweze kuja kutumika katika mpango mkakati ndani ya kipindi cha mwezi March na hatimae kuwasilishwa mwezi wa April kwa wataalamu wa ndani

Nae kiongozi wa wataalamu hao Paul Watkis ameahidi kuiwasilisha rasimu hio ya utafiti ili Zanzibar iweze kupanga mipango na mikakati yake yakukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi katika nyanja za kiuchumi .

Watkis pamoja na ujumbe wake wameelezea kuridhishwa kwao kutokana na mashirikiano mazuri waliyoyapata kutoka kwa wadau mbali mbali ambapo mawazo yao wameweza kufanikisha kufikia kwa baadhi ya malengo ya ukusanyaji wa tafiti ya rasimu hio wanayoiyandaa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.