Habari za Punde

Waziri Samia Atembelea Ujenzi wa Chuo cha Sayansi Bahari


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassani akitembelea Ujenzi wa Jengo la chuo cha Taasisi ya Sayansi ya Bahari kilichopo Chukwani Wilaya ya Magharibi Mkoa wa Mjini Unguja Kulia Mkurugenzi wa Taasisi ya Sayansi za Bahari Dk Margareth kyewalyanga[Picha na Ali Meja]


Waziri wa nchi afisi ya Rais anaeshughulikia masuala ya muungano Tanzania muheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewataka watumishi wanaofanyia kazi sekta ya muungano kuwa waadilifu kwani sekta hizo zipo kwa manufaa ya watanzania wa nchi mbili .

Hayo ameyasema leo kwa nyakati tafauti katika ziara yake ya kutembelea sekta za muungano hapa Zanzibar ili kuona utendaji wake wakazi na kujifunza yale wanayoyafanya katika utumishi wao .


Amesema sekta ya muungano ipo katika muundo wa nchimbili ambao kila mamoja anahitaji kufanikiwa katika sekta mbali mbali ikiwemo masuala ya usafirishaji na biashara ambao ndio mafanikio makubwa ya nchi na wananchiwake,amesema iwapo uadilifu utasimamiwa vyema kutaondoa malalamiko katika pande hizo mbili na hasa kwa wanasiasa na wananchi wao .

“Kuna haja kutao elimu kwa wafanya biashara wadogowadogo na wana siasa wawakilishi kuwaeleza kwa undani usahihi wa kodi ,sera za kodi ili waondoshe kero na malalamiko kwa wanachama wao”alisema samia .

Aidha waziri huyo alizipongeza sekta hizo kwa utendaji wao wa kazi na kusema kuwa ameridhishwa na utendajiwao kwani hivisasa kunaonekana mafanikio katika sekta hizo kwa kiasi na kusema kuwa changamoto zilizopo atazichukuwa na kuzifanyia kazi .

Nae naibu kamishina kwa upande wa mamlaka ya mapato Tanzania kanda ya zanzibar Mcha Hassan Mcha alizitaja baadhi ya changamoto katika bodi hiyo kuwa Zanzibar hakuna utaratibu wa kulipa kiwango maalumu cha kodi kwa wafanyabiashara wadogo wadogo kutokana na kikwazo cha sheria cha mwaka 1996 sheria namba sita ambapo usimamizi wa wafanya biashara wadogo wadogo unakua mgumu .

Pia alisema sheria za kodi ya mapato na sheria ya forodha ni moja lakini zina fanyakazi katika nchi mbili tafauti za jamhuri ya muungano wa Tanzania zenye mazingira tafauti ya kisasa kijamiii na kiuchumi mfumo huu unaleta changamoto nyingi katika usimamizi na utekelezaji

Pia alisema ni vigumu kuweka uwiano unaokubalika katika biashara ya kimataifa baina ya mdhibilti na ufanikishaji iwapo udhibiti wa idara ya foradha una kuwa mkubwa, wadau wa Zanzibar wanalalamika kuwa idara inachelewa utoaji wa mizigo inaweka mazingira magumu ya biashara na wawekeazji na iwapo idara itaelemea kwenye ufaninikishaji wadau wengine katika uchumi wanalalamika kuwa idara inavujisha mapato ya serikali na kuhatarisha usalama wa nchi na utumiaji bidhaa.

Aidha alisema zaidi ya asilimia 60 ya mapato ya TRA zanzibar yanatokana na kodi inayotokana Biashara ya kimataifa, hali ambayo biashara ya kimataifa haiaminiki kwa asilimia kubwa mtikisiko mdogo kwenye mtiririko ya Biashara ya kimataifa unao sababishwa na matatizo yote yakiwemo ya kiuchumi ,siasa kijamiina utendaji yanaleta athari kubwa katika ukusanyaji wa mapato ya TRA Zanzibar


“Kodi ya biashara ya kimataifa haitabiriki inategemea uingiaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi ambao nao hautabiriki”alisema Mcha

TRA anzibar imeasisiwa kwa sheria namba 11 ya mwaka 1995 na kuazza kutekeleza majukumu yake julai 1996 miaka iliopita ambayo inawafanyakazi wapatao 135 kwa hapa Zanzibar

1 comment:

  1. Ndio mammy! mwedo huo huo,..ukija 'ukidata' na sisi tuambulie chochote.
    Maneno ya Malika, naona manahoza wanagombania sukani

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.