SHIRIKISHO la Soka barani Afrika (CAF), limeifungia klabu ya Nania FC ya nchini Ghana kushiriki mashindano ya kimataifa kwa miaka mitatu baada ya kujitoa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho katika dakika za mwisho.
Nania ilijiondoa kucheza mechi ya marudfiano mwezi uliopita, siku mbili kabla siku iliyotarajiwa kupambana na wenyeji wao Sequence FC ya Guinea katika mzunguko wa awali wa mngarambe hizo.
Ikichukua uamuzi huo, Nania ilisema sababu kubwa ya kufanya hivyo, ni kujitoa kwa mdhamini wake mkuu, na kuiacha timu hiyo bila ya fedha za kutosha kuiwezesha kushiriki katika kampeni za kuwania kombe hilo.
Mbali na kutupwa jela kwa kipindi hicho, klabu hiyo pia imepigwa faini ya dola 500 za Kimarekani.
Klabu hiyo iliyoasisiwa na kufundishwa na awali na nyiota wa zamani wa Ghana Abedi Pele, ilikuwa timu ya kwanza ya daraja la kwanza kushindakombe la ligi nchini Ghana.
No comments:
Post a Comment