Habari za Punde

Innaa Lillaahi Wainnaa Ilayhi Raaji'uun - Mnikulu Zanzibar Hatunae Tena ni Shaaban Hilika



MNIKULU katika Ikulu ya Zanzibar, Shaaban Ahmada Hilika, amefariki dunia leo katika hospitali ya Mnazimmoja alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

Hilika anatarajiwa kuzikwa kesho katika kijiji cha Mfenesini  baada ya Sala ya Adhuhuri, na mwili wa marehemu utaondokea Amani  nyumbani kwao, baada ya kuagwa na kusaliwa..

Hilika amekuwa Mnikulu katika Ikulu ya Zanzibar tokea uongozi wa Awamu ya Sita ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Dk.Amani Abeid Karume na kuteuliwa tena kushika nafasi hiyo na Rais wa Awamu ya Saba wa Zanzibar, Dk.Ali Mohamed Shein.

Mungu ailaze mahali pema roho ya marehemu, Amin.

6 comments:

  1. Innalilah wainna ilahi rrajiuna,inshaallh M/Mungu atawapa subra wafiwa

    ReplyDelete
  2. Mungu akujaalie kauli na akulaze malaha pema peponi . Innalilaah Wan inaillihil rajiiuna.

    ReplyDelete
  3. You were the best human being on earth...May God rest your soul in peace. Our Heartiest condolence to the family

    ReplyDelete
  4. Inna lil-lahi, Wainna ilaihi raji'uun!
    Kwa mujibu wa hii picha,inaonekana aliugua sana jamaa, nnavyomkumbuka alikua mnene na mwenye afya.
    Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi..Amin.

    Kaka mapara usichoke kutuhabarisha matukio ya kwetu kwa kweli tuna kutegemea sana.
    Juzi juzi, ulitokea msiba wa mtu mzito hapo, tukapeana moyo kwamba Mapara atatuhabarisha lakini wapi!

    Ulikua ni msiba wa Bw. Wolfong Dorado, ingawa alikua ni Goa kwa asili na Mkristo kwa imani bado tunaamini, ni Mzanzibari na ktk uhai wake alishika nafasi nyeti na hadi anafariki kama sikosei alikua mtumishi wa umma.

    Sisi tunaamini Wazanzibari wa aina hii(minority) ndio wenye uwezo wa kuitendea haki Z'bar kwa vile hawana 'shamba' hapa wala watu wakuwapendelea, na kweli Dorado alikua mwaminifu!

    ReplyDelete
  5. anony wa tatu shukran kwa maoni. Mbona Maziko ya Dourado tumeyaweka kwenye blog au ulikusudia taarifa ya kifo chenyewe?

    ReplyDelete
  6. Duu, kaka samahani na ahsante kwa taarifa!
    Kweli nimeona kwenye 'older posts' kuna picha safi na za kutosha, na Wazanzibari kama kawaida wameonyesha ushirikiano wa kutosha utadhani sio mtu wa imani tofauti?

    Inaonyesha kila tukenda mbele 'uhadimu na uhafidhina' unazidiwa nguvu!
    Kazi njema kaka.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.