Habari za Punde

Kutahiri Kunaweza Kupunguza Ugonjwa wa Saratani ( Prostate Cancer)

Kutahiri kunaweza kupunguza idada ya wanaume wanaosemekana kuugua ugongwa wa Saratani kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Wanasayansi katika kituo cha Fred Hutchinson Cancer Research Centre, Seattle, Marekani.

Wanasayansi waliweza kubaini kwamba wanaume waliotahiriwa kabla ya kuanza kufanya tendo la ndoa walikuwa na nafasi ndogo zaidi ya kuathrikia na Prostate Cancer kuliko wawaume wasiotahiriwa kwa tofauti ya asilimia 15.

Utafiti huu ambao ulijumuisha takriban wanaume 3399 ambapo nusu yao walikuwa tayari wana ugonjwa na wengine hawakuwa na ugonjwa.


Hata hivyo wanasayansi wamesema kwama hii ni hatua ya mwanzo katika utafiti huu  na hivyo isichukuliwe kama umekamilika na wataendelea zaidi katika kuona vipi Wanaume waliotahiriwa wanaweza kuepukana na athari za saratani hii ambayo huwakumba wanaume wengi duniani.


Ndipo hapa tunaporudi kwenye asili ya dini zote za Allah Subhaanahu Wata'ala na pia dini  yetu ya kiislamu ambapo jambo hili limekuwa ni lazima kufanyiwa kwa mtoto anapozaliwa.

Manufaa yake ni mengi kuna tunayoyajua a mengine tusiyoyajua kama haya ambayo ndio kwanza yameanza kugundulika baada ya kufanyika tafiti hizi za kisayansi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.