Mchezaji wa timu ya Black Sailor Bakari Kuluzo (katikati) akimpita beki wa timu ya Vikokotoni Pharmacy, katika mchezo wa ligi daraja la kwanza uliofanyika uwanja wa mao timu hizi zimetoka sare ya 1--1.
Hivi ndivyo ilivyokuwa katika mchezo wa marudiano kati ya Black Sailor na Vikokotoni Pharmacy, baada ya mchezo wao wa awali kufutwa kwa, uliofanyika kiwanja cha ngome Fuoni, timu ya Viko ilikuwa imeshinda 1--0.leo zimetoka sare ya 1--1.
Mdau na wewe unaweza kuruka kama hivi? Beki wa timu ya Black Sailor Muhidini Yussuf, akiokoa moja ya mpira eneo la gali lake.
Wachezaji wa Viko Pharmcy wakishangilia goli lao katika kipindi cha kwanza cha mchezo wa ligi daraja la kwanza Zanzibar.
Mshambuliaji wa timu ya Black Sailor Hassan Jabir kushoto akimpiga chenga beki watimu ya Viko Pharm Hassan Omar, katika mchezo wa ligi daraja la kwanza, uliofanyika uwanja wa Mao timu hizo zimetoka sare ya 1--1
No comments:
Post a Comment