Brigedia Jenerali, Adam clement Mwakanjuki wakati wa uhai wake akisalimiana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika hospitali ya Lugalo Jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa Waziri wa zamani wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Brigedia Jenerali, Adam clement Mwakanjuki amefariki dunia katika hospitali ya Lugalo Jijini Dar es Salaam. Marehemu Mwakanjuki amefariki duani jana Alaasiri baada ya kuugua kwa mfupi. Hata hivyo haikuelezwa alikuwa akisumbuliwa na kitu gani lakini alifikishwa hospitalini mapema wiki hii.
Brigedia Jenerali Mwakanjuki ni miongoni miongoni mwa wanasiasa wakongwe hapa nchini ambaye alianza kazi ya siasa kabla ya mapinduzi ya Zanzibar ya januari 12, 1964 katika chama cha Afro shirazi (ASP) na baadae Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Marehemu Mwakanjuki aliwahi kuwa waziri wa kilimo na mifugo, waziri wan chi ofisi ya rais katiba na utawala bora, waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za miko na vikosi vya SMZ na mumbe wa baraza la wawakilishi kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa familia ya marehemu wamesema kwamba taarifa ya mazishi itatolewa leo baada ya kukutana wanafamilia hiyo visiwani Zanzibar.
“Ni kweli Mjomba amefariki hivi punde dare s salaam na mipango ya mazishi itapangwa baada ya kikao cha familia yetu” alisema Vicky Mwakanjuki mtoto wa Dada wa Marehemu.
Wakati wa uhai wake Marehemu Mwakanjuki alikuwa waziri mwandamizi katika serikali ya Zanzibar katika wizara mbali mbali pamoja na kuwa mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya CCM (NEC).
Tangu mwaka 2007 Marehemu Mwakanjuki hakuonekana katika harakati za siasa baada ya kupata ajali mbaya akitokea Dodoma kwenda Dar es Salaam katika eneo la Morogoro ambayo ilisababisha kuvunjika sehemu zake za viungo.
Licha ya juhudi za kupatiwa matibabu ndani na nje ya nchi lakini hakuweza kurudi katika hali yake ya kawaida ambapo wakati wa tukio inatokezea alikuwa akiendesha gari lake mwenyewe pamoja na mwanawe.
Mwakanjuki pia alikuwa afisa mwandamizi katika jeshi la wananchi wa Tanzania na kufikia cheo cha Brigedia Jenerali na ameongoza brigedi mbali mbali ikiwemo pia kuwa miongoni mwa waanzilishi wa jeshi la kujenga taifa JKT.
Hadi kufikia mwaka 2010 Marehemu alikuwa waziri wa mawasiliano a uchukuzi Zanzibar pamoja na kuwa mjumbe wa NEC hadi mauti yanamkuta.
Mwenyezimungu amlaze mahali pema marehemu Adam Mwakanjuki.
ReplyDeleteKwa ufupi marehemu Adam Mwakanjuki hakuwa mwanasiasa tuu bali alikuwa ni mwanaharakati wa kupigiwa mfano katika harakati za chama cha wafanyikazi hapa Zanzibar katika miaka ya mwisho ya 1950's hadi yalipotokea mapinduzi Zanzibar.
Wenzake katika harakati hizo ni kina Hassan Nassor Moyo, Ahmed Diria Hassan, Jimiringo, Kadiria Muyeji na wegineo ambao wengine bado wako hai na wengine wameshatangulia mbele ya haki na Mwenyezimungu awarehemu, Ameen.
Halkadhalika, kama sikosei marehemu Adam Mwakanjuki pia alikuwa na ushirikiano mkubwa na viongozi wa vyama vyengine vya wafanyakazi vilivyo kuwepo Zanzibar wakati huo kabla ya Mapinduzi kwa mfano Bw. Khamis Abdulla Ameir (ambapo nakupeni siri leo waliwahi kumbatiza wakimwta COMRADE).Ningeliwaomba waandishi wamfuate Bw. Khamis Abdulla Ameir ili aweze kuwasaidia kuwapa historia ya jemedari Adam Mwakanjuki katika harakati za vyama vya wafanyakazi Zanzibar.
Kwa bahati mbaya muda mfupi baada ya Mapinduzi kulitokea switafahamu kati ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar marehemu Abeid Amani Karume na kina Adam na Jimiringo. Adam Mwakanjuki alihamia Mrima na kwabahati nzuri siku moja marehemu Raisa Nyerere alipokua katika ziara zake Mikoani akifatana na Waziri wake marehemu Abdulrahman Babu, marehemu Babu alimuona Adam akiwa katika hali ambayo hakustahili na ndipo walipomchukua Dar na marehemu Nyerere kumpa Ukuu wa Wilaya kabla ya kuhamishiwa katika Jeshi la Kujenga ambako alonesha miujiza ya uchapaji kazi.
Leo marehemu Adam Mwakanjuki ametutoka lakini akina sisi watu wa umri wake hatutomsahau na Mwenyezimungu amlaze mahali pema huko mbele ya haki, ameen.
Muandishi Mapara, tafadhali watafute Mzee Hassan Nassor Moyo na Khamis Abdula Ameir ili wakupatie historia ya jemedari huyu ili utuandikie 'ORBITUARY' ya marehemu
Mtoa maoni tunakushkuru kwa kutupa profile ya Marehemu Mwakanjuki, na mimi pia namkumbuka akiwa Utawala bora moja katika sifa zake ni kuwa alikuwa si mtu ambae alikuwa akikubali majungu na ubaguzi ingawa wakati ule wa Rais Dr Salmin yalikuwa yamepamba moto, Allah amuweke anapostahiki
ReplyDeleteWachangiaji wa hapo juu, inaonyesha wazi kuwa neno marehemu linakupigeni chenga katika kulitumia.
ReplyDeleteTuelimishe otherwise na wewe hulijui pia
DeleteMchangiaji hapo juu, ingelikuwa jambo la maana ukawasomesha hao wachangiaji waliokutangulia jinsi ya kulitumia hilo neno 'MAREHEMU' kwani akina sisi hahe hohe tusiokielewa Kiswahili cha kisasa cha Msamiati tunaona ni sawa tu.
ReplyDelete