Habari za Punde

Dk Shein Apewa Taarifa za Halmshauri za Mkoa wa Kusini Pemba

Na Khamis Mohammed Maelezo , Pemba

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Permba Meja Mstaafu Juma Kassim Tindwa amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Mkoani imekusanya jumla ya shs Millioni 44 lakini tano na sitini elfu na Halmashauri ya Wilaya ya Chake chake imekusanya jumla ya shs Millioni 34 laki nane kuminatatu elfu mia mbili na moja.

Amesema kuwa fedha hizo zimetumika kwa shughuli za maendeleo kama ujenzi wa bara bara, Soko la Mkanyageni na kituo cha uwalimu katika wilaya ya Mkoani ambapo katika Wilaya ya Chake chake shs Millioni 6 laki tatu tisini na tano elfu na mia tisa kwa ujenzi wa kituo cha Afya na Matayarisho kwa ujenzi wa Halmashauri na ukarabati wa njia.


Meja Mstaafu Juma Kassim Tindwa alieleza hayo huko katika ukumbi wa Chuo cha Amali Vitongoji wakati alipokuwa akiwasilisha ripoti ya utekelezaji ya Mkoa wake mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein ambapo pia wananchi na Viongozi mbali mbali walihudhuria.


Akielezea juu ya Baraza la Mji la W ilaya ya Mkoani Tindwa amesema jumla ya shs Millioni 31 laki mbili na thalathini na tatu elfu na Hamsini zimekusanywa ambapo Wilaya ya Chake Baraza limekusanya jumla ya shs Millioni 68 laki nne elfe tisa mia tisa na sita kwa kipindi hicho.


Fedha hizo zimepatikana kutokana na vianzio mbali mbali vya mapato yakiwemo leseni za Biashara mbali mbali.

Akizungumzia kuhusu kilimo cha Mpunga Tindwa amesema kuwa jumla ya ekari 7773. zimelimwa katika Mkoa huo na kuvukwa kwa lengo lililowekwa.

Pia katika taarifa hiyo Tindwa ameelezea juu ya mafanikio mbali mbali yaliofikiwa na Mkoa huo pamoja na Changamoto zinazoukabili Mkoa katikia sekta mbali mbali zikiwemo Elimu,Afya, Biashara,Mifugo na njia ambazo Serikali katika Mkoa huo imekusudia kukabiliana nazo.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO PEMBA

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.