Na Jumbe Ismailly, SINGIDA
WATU watatu wamefariki dunia katika matukio tofauti Mkoani Singida, likiwemo la mzee mwenye umri wa miaka 70, mkazi wa kijiji cha Magugumaji wilayani Iramba, kuuawa na ndugu zake wakidai kuchoka kumuuguza.
Mzee huyo aliyeuawa ametambulika kwa jina la Daud Mrangi (70), na kwamba aliuazwa na jamaa zake kwa kile walichodai kuwa ni kero ya kumuuguza kwa muda mrefu hadi kupata upofu wa macho.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Singida, SACP Celina Kaluba alisema kuwa tukio hilo lilitokea Aprili 02, mwaka huu majira ya saa 11:00 jioni nyumbani kwake katika kijiji cha Mmagugumaji, kata ya Ndago, wilayani Iramba.
Aidha Kamanda huyo wa polisi baada ya mzee Mrangi kukutana na dhahama ya kukatishiwa maisha yake, mwili wake ulikutwa ukiwa na majeraha sehemu ya mgogoni na michubuko kwenye mkono wake wa kushoto huku akitokwa na damu mdomoni na puani.
Alisema kwamba chanzo cha mauaji hayo ni ndugu zake kuchoka kumuuguza na kwamba marehemu huyo aliugua katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili.
Alifafanua kuwa na katika kipindi cha muda huo, alipopata upufo, ndugu zake wakaamua kumuua ili waweze kuondakana na kero ya kumuuguza.
Alibainisha kamanda huyo kuwa kufuatia tukio hilo wanamshikilia Magreth Omari (50) na Shabani Hassani (21) kwa tuhuma ya mauaji ya mzee Mrangi, na kwamba upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma ya mauaji hayo.
Katika hatua nyingine Kamanda Kaluba alisema mkazi mmoja wa mtaa wa Unyankindi, katika Manispaa ya Singida Seif Zakaria (20), amefariki dunia baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira na kisha kuchomwa moto kwa tuhuma ya kuiba pikipiki.
Kwa mujibu wa msemaji huyo wa jeshi siku ya tukio mtuhumiwa Seif alikodi pikipiki yenye namba za usajili T.315 BXP aina ya fekon iliyokuwa ikitumiwa na dereva, Iddi Juma kwa shughuli za kusafirisha abiria.
Alisema mtuhumiwa huyo alipokodi usafiri huo alitaka apelekwe katika Kijiji cha Sepuka na haikufahamika alikuwa atozwe kiasi gani, lakini hata hivyo alitoa noti ya shilingi 10,000 na dereva wa pikipiki hiyo akaenda kutafuta chenchi huku akiwa ameacha ufunguo wa pikipiki kwenye pikipiki hiyo.
“Mtuhumiwa alitumia uzembe wa Idd kuacha ufunguo wa pikipiki na ndipo alipoiwasha na kuanza kutoroka nayo akielekea barabara ya Singida – Sepuka, na kwamba hata hivyo alipofika katika kijiji cha Ititi, kwa mbele aliona kundi kubwa la watu wenye pikipiki na kuamua kuigeuza kurudi Singida mjini”, alifafanua Kamanda Kaluba.
Alisema kamanda Kaluba kuwa mtuhumiwa Seif alipofikishwa katika eneo alikopora pikipiki hiyo,alikuta kundi la wananchi wenye hasira kali wakimsubiri na ndipo walipoanza kumpiga kwa silaha za jadi.
Alifafanua kamanda kuwa wakati akiwa bado yu hai wananchi hao waligema petroli iliyokuwa kwenye pikipiki aliyoiiba na kumwagia na kisha kumchoma moto.
Alisema hata hivyo polisi wapofika kwenye eneo la tukio na kukuta akiwa anaungua moto na huku akiwa bado yuhai, na ndipo walimchukua na kumwahisha kwenye hospitali ya Mkoa na alifariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa hapo hospitalini.
Wakati huo huo Bi Kaluba alisema Shamu Seif (28) mkazi wa Mtaa wa Majengo mjini Singida, amefariki dunia baada ya gari alilokuwa akisafiria kuacha njia na kisha kupinduka katika barabara ya Singida – Ilongero.
“Ajali hii inayohusisha fuso lenye namba za usajili T.890 AGT mali ya Bwana K.J.Kavishe mkazi wa mjini Singida,ilitokea juzi saa tisa alasiri,na kwamba Hemedi Abdu (25),Athumani Majii (28),Muhusini Bakari (25),Azizi Hassani (38) na Juma Maulidi (18),wamejeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao”,alisema Kamanda Kaluba.
Alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa fuso hilo ambalo dereva wake hajafahamika jina lake na ametoroka baada ya kutokea kwa ajali hiyo,na msako mkali unaendelea ili kumnasa aweze kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
No comments:
Post a Comment