Habari za Punde

Konde Stars Yaishtaki ZFA

Na Masanja Mabula, Pemba

KLABU ya soka ya Konde Stars imepiga hodi katika ofisi za Kamati ya Rufaa na Usuluhishi ya ZFA kupinga maamuzi ya kamati tendaji ya chama hicho Taifa Pemba kuipokonya ushindi na kuizawadia timu ya Majimaji ya Tumbe.

Konde Stars ambayo kwa sasa imeshuka daraja kutoka ligi daraja la kwanza Taifa msimu huu, imechukua hatua hiyo kudai irejeshewe pointi zake hizo ili iweze kubaki katika daraja hilo.


Mmoja wa viongozi wa timu hiyo Masoud Seif, ameliambia Zanzibar Leo kuwa, uamuzi wa kamati tendaji dhidi ya timu yake umefanywa kimakosa kwa kuwa wao hawakushirikishwa kwenye kikao kilichotoa maamuzi hayo.

Konde inayotoka Wilaya ya Micheweni sambamba na Majimaji, zote zimeshuka daraja ambapo msimu ujao zitashiriki ligi daraja la pili Taifa Pemba.

Awali, ZFA iliinyang’anya ushindi timu hiyo baada ya kukatiwa rufaa na Majimaji ikidaiwa kuchezesha mchezaji Mohammed Nsajigwa ambaye hakusajiliwa kihalali.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.