Habari za Punde

‘May Day Cup’ Mwendo Mdundo

Na Asya Hassan

TIMU ya maofisa wa uwekezaji na vitega uchumi Zanzibar ZIPA, wamewatambia wajenga uchumi wa JKU, kwa kuwafunga magoli 2-1 katika mfululizo wa mechi za tamasha la Mei Dei zinazochezwa uwanja wa Amaan nje.

Na katika mchezo mwengine, mabaharia wa KMKM wakawaadhiri maofisa wa pasipoti timu ya Uhamiaji kwa kichapo cha magoli 3-2.


Mapema juzi, maafande wa Polisi waliwatoa nishai vijana wa Dk. Shein timu ya Ikulu kwa kuwafunga mabao 3-2.

Aidha watunga sheria wa Baraza la Wawakilishi wakawafundisha soka wazee wa kesi timu ya Mahakamani kwa kuwatandika mabao 2-0.

Kwa upande wa mpira wa wavu, timu ya Mafunzo ikawachezesha gwaride maafande wa Polisi kwa kuwafunga seti 3-0, huku Darajani ikawazamisha vijana wa Zenj FM kwa mabao 3-1.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.