Na Khamisuu Abdallah
SHEHA wa Shehia ya Miembeni mjini Zanzibar, Haji Shomari Haji jana alikuwa na kazi ngumu ya kuwatulizanisha waumini wa dini ya kiislamu na kikristo ambao walikuwa wakiwania kiwanja kwa ajili ya kufanyia ibada.
Akizungumza na gazeti hili, Sheha huyo alisema alilazimika kuzungumza na kila upande na hatimeye kufikia muafaka juu ya matumizi ya kiwanja hicho ambacho kipo karibu na Madrasa na kanisa la Depar Christianity Life.
Alisema waumini wa kiislamu katika madrasa iliyopo karibu na kiwanja hicho jana walijipangia kusoma maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W), ambayo husomwa kila mwaka katika madrasa hiyo.
Kwa upande mwengine wakiristo nchini kote wako kwenye sikukuu ya pasaka ambao nao pia walidhamiria kukitumia kiwanja hicho kilichopo Muembe Madema kwa ajili ya shughuli zao.
Hata hivyo Sheha huyo alisema makubaliano yalifikiwa ambapo uongozi wa madrasa hiyo ulikubali kufanya maulidi yao wakati wa usiku na waumini wa dini ya kikiristo kufanya ibada yao kuanzia saa 10:00 mpaka saa 12:00 jioni.
Alisema kuwa baada ya kutokea mtafaruku huo aliwaita viongozi wote wa pande zote mbili na kukubaliana kwa kuepusha ugomvi ambao hauna msingi wowote kwa maslahi ya nchi.
Sheha huyo alisema Zanzibar nchi isiyo na sifa ya mizozo ya kidini na hivyo kuwataka waumini wa dini kuvumiliana na kufanya maamuzi ya busara pale hitilafu zinapotokea.
heh znz ambayo tumeiwacha sisi hakuna kafiri anaefanya mambo yao hadharan zaid ya makanisani ambayo ilikuwa tunayajua kwa hesabu.Sasa nasikia hata idadi hayajulikani.YAA RABBI INUSURU ZANZİBAR NA KINUSURU KIZAZI CHA WAZANZIBAR NA MBINU ZA MAKAFIRI.
ReplyDeleteRabbi hawezi kuinusuru Zanzibar na ujio wa wakristo. Viongozi wanawaachia waje, sasa wakija wanakuja na dini zao. Wakija na dini zao inabidi wapate mahali pa kufanyia dini zao. Sasa Mungu ainusuru Zanzibar na nini wakati "tumeyataka wenyewe ilobaki shauri yao?"
DeleteNa bado huu ndio mwanzo watataka kila wanachokifanya Tanganyika na Zanzibar wakifanye. Viongozi wetu ni woga sana kwasababu wanafikiri kuwa kama si CCM bara basi na wao hawana kazi
matamu hapa tkwa kila alie chimba kisima twasubiri waingie au mtii hawao jamaa unaarudia
ReplyDeletemwisho
ukicheza na mbwa atakufuta hadi msikitini ni haki yao!
Nimtihani mkubwa kwa zanzibar yetu kufikia halii hii.tuzinduke wazanzibar sisi ndo waathirika.
ReplyDeletekwa vyovyote vile wakulaumiwa ni serikali ..wanatoa viwanja vijengwe makanisa hao wakiristo wa zanzibar wanajulikana kwa idadi hayo makanisa ya mkunazini na minara miwili hawaji sasa kisa cha kutoka kiwanja ni makusudi ni mbinu za watanganyika watutawale kifikra, waislamu tuungane kuliondoa hilo kanisa hapo ikiwezekana hata nguvu itumike
ReplyDeleteHakuna lawama kwa serikali ikiwa miaka yote hii hamujaona atahri za CCM ndio hizi subirini watoto wenu wabakwe na Wagalatia ndio mutauona umuhimu wa kupiga kura na kueka serikali itakayolinda maadili.
ReplyDeleteKwa mtaji huu, naona hatutoki!
ReplyDeleteYaani pamoja na miaka 38 ya elimu bure hadi chuo kikuu, watu wanashindwa kujua athari za kuishi ktk 'globalising world'
Kwa kweli naona mawazo ya udini yamezidi utadhani sisi hatuishi kwa wenzetu kwa uhuru.
Watu leo hii wanaona fakhari, wao ua vijana wao kuishi ktk nchi za Ulaya na Marekani huku wakielezea uhuru wa kidini walionao, utawasikia wakisema;.. london kuna bonge la msikiti!