Wananmchi waliofika katika kituo cha kutoa huduma ya Mafuta ya Petroli katika kituo cha Kijangwani wakishanga jinsi mashine hiyo ikiwa imeanguka chini kutoka mahali pake pa kawaida ikitowa huduma kwa wateja wanaifika kituoni hapo
Mkasa huu umetokea katika kipindi cha saa nane za mchana wakati mteja akifuata huduma ya mafuta kituoni hapo, na baada ya kupa huduma hiyo ya mafuta ya petroli ilibdi aondoke bila ya kujuwa kama muhudumu wa kituo hicho amemaliza kutia mafuta.
Doo salale sijuwi tumlaumu nani katika mkasi huo kumbe muhudumu wa kituo hicho amechelewa kutoa mkonge wa mafuta na derevye huyu kuondosha gari yake na kuifta mashine hiyo hadi chini kuacha sehemu yake ikiwa wazi
Mungu ameleta kheri yake bila ya kutokea maafa na kujeruhiwa kwa mtu kutokana na ajali hiyo, mashine hiyo ikiwa imewekwa bila ya kufungwa na nati ili kuiziiya isije ikapata misukosuko kama hii,
Inabidi wamiliki wa Vituo vya kuuzia mafuta wachukuwe tahadhari ya makusudi kuzifunga mashine kuzuiya yasije yakatokea kama hayo na kuleta balaa kwa Wateja wanaofuata huduma hiyo katika vituo vya kuuzia mafuta ya Petroli.
No comments:
Post a Comment