Rais Jakaya Kikwete na viongozi wenzake wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakitia saini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano katika ulinzi wa nchi hizo leo Aprili 28, 2012 katika hoteli ya Ngordoto jijini Arusha.
Rais Jakaya Kikwete na viongozi wenzake wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakionesha hati baada ya kutia saini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano katika ulinzi wa nchi hizo leo Aprili 28, 2012 katika hoteli ya Ngordoto jijini Arusha.
Viongozi Wakuu wa Jumuiya ya Afrika mashariki Wakitia Saini Mkataba wa Makubaliano ya kuwa na Ulinzi wa Pamoja wa Nchi Wananchama wa Jumuiya hiyo.
Picha ya pamoja ya Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki {EAC } waliokutana katika Hoteli ya Ngurudoto Mjini Arusha kaika Mkutano wa 10 wa Jumuiya hiyo. Wanne walioka kutoka Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Rais Mwai Kibaki wa Kenya.
Na Othman Khamis Ame
Maendeleo ya haraka sambamba na kujikwamua Kiuchumi kwa Mataifa yanayounda Jumuiya ya Afrika ya Mashariki { EAC } yatapatikana endapo Nchi hizo zitajizatiti katika kuwekeza katika Sekta ya Miundo mbinu hasa ile ya Mawasiliano ya Bara bara.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Mwai Kibaki wa Jamuhuri ya Kenya wakati akizungumza kwenye Mkutano wa 10 Viongozi Wakuu wa Jumuiya hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Meru katika Hoteli ya Ngurudoto Mkoani Arusha.
Bwana Kibaki alisema Mfumo wa Miundo Mbinu uliopo ndani ya Mataifa Wanachama wa Jumuiya hiyo bado unaendelea kuwa vikwazo kwa Mataifa hayo kuelekea kwenye Maendeleo ya Haraka. Mwenyekiti huyo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki alifahamisha kwamba yapo matatizo mengi katika sekta ya mawasiliano ya bara bara jambo ambalo linaviza kwa kiasi kikubwa kasi ya Kiuchumi.
“ Tumeshuhudia zaidi ya asilimia 90% ya Wananachi wa Mataifa yetu haya wanatumia Bara bara ambao hauridhishi katika harakati zao za Biashara na Mawasiliano” Alisisitiza Rais Kibaki katika Mkutano huo.
Aliwaagiza Vionozi na Watendaji wa Jumuiya hiyo kuhakikisha kwamba upo umuhimu wa suala hilokutilia mkazo zaidi katika vikao vijavyo vya Jumuiya hiyo kwa lengo la kuona tatizo hilo linapatiwa ufumbuzi.
Akizungumzia Suala la Somalia na Sudan ya Kusini kuomba Uanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Mwenyekiti huyo wa Jumuiya hiyo Rais Kibaki alieleza kwamba Uongozi wa Jumuiya hiyo bado unaendelea kuzingatia zaidi ombi la Nchi hizo ili hstimse kutoa Maamuzi muwafaka.
Alisema yapo masuala kadhaa yanayojadiliwa kuhusiana na Maombi hayo, lakini kinachozingatiwa zaidi ni upatikanaji wa hali ya amani na Utulivu wa Mataifa hayo. Kuhusu suala la soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki Mwenyekiti Kibaki aliwaagiza Mawaziri wa Fedha wa Nchi Wanachama kuharakisha kazi waliyopewa ili kuona dhana ya kuanzishwa kwa soko hilo inafikiwa.
Alisema Wananchi walio wengi ndani ya Jumuiya hiyo bado wanashauku ya kutaka kuona ile ndoto ya kuwa na forodha moja ndani ya Afrika Mashariki inafikiwa.
Mapema Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Balozi Dr. Richard Sezibera alisema kumekuwa na Maendeleo makubwa ndani ya kipindi cha Miaka 11 hasa katika sekta ya Biashara na Mawasiliano.
Dr. Richard alisema katika kipindi cha mwaka 2011 hadi 2016 Jumuiya hiyo imelenga kujenga nguvu zaidi katika masuala ya Uchumi na Maendeleo ya Wanajumuiya.
Mkutano huo pamoja na Mambo mengine uliwawezesha Marais wa Mataifa hayo Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutia Saini Mkataba wa Ulinzi wa pamoja wa Nchi zinazounda Jumuiya hiyo.
No comments:
Post a Comment