Msanii Mohd Ahmed pia
ni Mlezi wa Kikundi hicho Maarufu hapa Zanzibar
katika kutoa burdani ya Muziki wa Taarab wa kisasa.
Makamu wa Pili wa
Rais wa
Kulia yake ni
Mkurugenzi wa Kikundi hicho Ustaadhi Abdulla Ali { Maarufu kwa jina
la Du }.
Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wasanii wa Kikundi cha
Zanzibar One Taarab kwenye sherehe za kutimia Miaka Mitano tokea kuanzishwa kwa
Kikundi hicho huko Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya pamoja na Wasanii
wa Zanzibar One Taarab katika sherehe za kutimia Miaka Mitano tokea kunzishwa
kwa Kikundi hicho hapo katika Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar.
Wakati umefika kwa Vikundi vya Sanaa Nchini kuendelea
kufanya kazi zao katika misingi ya Kibiashara ili kuwa na uwezo wa kujijengea
mazingira ya kujitegemea.
Kazi ya sanaa si ya kuipuuza wakati huu kwa vile tayari imeshaonyesha muelekeo mpana wa kutoa
ajira hasa kwa kundi kubwa la Vijana
katika sehemu mbali mbali Duniani.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi alieleza hayo katika sherehe Maalum ya kutimia Miaka Mitano tokea
kuasisiwa kwa Kikundi cha Taarab ya Kisasa Zanzibar { Zanzibar One Taarab } zilizofanyika
katika Ukumbi wa Salama Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar.
Sherehe hizo za aina yake zilizobeba wapenzi mashuhuri
wa Muziki wa Taarab ya Kisasa { Modern Taarab } zilipambwa na wimbo mzito wa
Mapenzi yangu pokea ulioghaniwa na Msanii Gwiji wa Sanaa ya Taarab Zanzibar
ambae pia ni Mlezi wa Kikundi cha Zanzibar One Taarab Ustaadhi Mohd Ahmed.
Akitoa nasaha zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif aliwapongeza Wasanii wa
Kikundi hicho kwa juhudi zao za kutoa Burdani na kuwaomba waendelee kudumu na
kuwa mahiri zaidi.
Alisema Vikundi vingi vya Sanaa huanzishwa vyema
lakini hatma yake hufifia kutokana na migogoro lakini inapendeza kuona Zanzibar
One Taarab bado inanawiri na kutamba.
“ Kikundi chenu kina Wasani wazuri kama kungekuwa na
tunzo naamini Kikundi hichi kingetokea mshindi. Kwa niaba yangu na Familia
yangu nawapa hongera kwa kutimia miaka
mitano. Happy
Birthday”. Balozi Seif alikifyagilia Kikundi hicho.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema kwa vile
Sanaa ni ajira mfano wa Wasanii wa Ulaya ipo haja kwa Washirika wa Fani hii
kuendelea kuunga mkono Kikundi kama hicho ili Vijana hao wawe na uwezo kamili
wa kuendesha Maisha yao.
Katika kuunga mkono juhudi za kikundi cha Zanzibar One Taarab
Balozi Seif ameahidi kukizawadia Shilingi 1,000,000/- Kikundi hicho ili
zisaidia kutunisha mfuko wake.
Akitoa shukrani kwa niaba ya Wasanii wenzake
Mkurugenzi wa Kikundi hicho cha Zanzibar One Taarab Ustaadhi Abdulla Ali
maarufu { Du } alisema lengo la kuanzishwa kwa Kikundi chao
ni kutoa
Burdani kwa Jamii kupitia Sanaa hiyo ya Taarab.
Mkurugenzi Abdulla Du amewapongeza Viongozi na
Washirika wao wote walioamua kujitolea kukisaidia Kikundi chao ambacho
hivi sasa kiko katika muelekeo mzuri.
Kikunci cha Zanzibar One Taarab kimeanzishwa Mwaka
2007 hivi sasa kikiwa na umri wa Miaka Mitano.
No comments:
Post a Comment