Habari za Punde

Kuwasili Mwili wa Marehemu Brigedia Mstaaf Adam Mwakanjuiki Zanzibar.

Ndege  iliobeba mwili wa Marehemu Bregedia Adam Mwakanjuki ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar mchana huu tayari kwa maziko saakumi Mwanakwerekwe .
Makamanda wa JWTZ  wakiushusha mwili wa Marehemu Brigedia Mstaafu Adam Mwakanjuki katika ndege ya Jeshi baada ya kuwasili Zanzibar kwa mazishi leo jioni.

Viongozi wa Serikali na Vyama vya Siasa  wakiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa  kuupokea mwili wa Brigedia Mstaafu  Adam Mwakanjuki.
Makamanda wa JWTZ  wakiwa katika mwendo wa pole wakitembea wakiubeba mwili wa Marehemu Mwakanjuki baada ya kuwasili Zanzibar kwa ajili ya Mazishi yanayofanyika leo jioni katika makaburi ya mwanakwerekwe Zanzibar.
Ndugu na Jamaa wakiwa katika uwanja wa ndege  wakisubiri kuupokea mwili wa marehemu asubuhi.





Askofu Mstaafu wa Kanisa la Mkunazini  John Ramadhani akiweka saini kitabu cha maombolezo katika ukumbi wa baraza la wawakilishi la zamani kikwajuni, sehemu ilioandaliwa kutowa heshima na kuuaga mwili wa marehemu.



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.