TATIZO la Zanzibar kutozalisha bidhaa za kutosha kwa mahitaji yake, kumechangia kuanguka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania.
Hali hiyo imesababisha Tanzania itumie fedha nyingi za kigeni, kununulia bidhaa kutoka nje.
Kauli hiyo imetolewa barazani na Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais, Fedha, Uchumi, Mipango ya Maendeleo, Omar Yussuf Mzee.
Waziri huyo alikuwa akijibu swali la Rashid Seif Suleiman (Ziwani).
Mwakilishi huyo alitaka kujua sababu za kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania.
Waziri huyo alisema Tanzania inakabiliwanauzalishaji mdogo wa chakula jambo ambalo limekuwa likiisababishia serikali kutumia fedha nyingi za kigeni.
Alisema sababu nyengine inayochangia halihiyo ni pamoja na kupanda kwa bei ya mafuta mara kwa mara, kuchafuka kwa masoko ya kifedha diuniani kunakosababishwa na matatizo ya kifedha hasa katika Bara la Ulaya.
Alisemamambo hayo pamoja namengine yanachangia kuporomoka kwa thamaniya shilingi ya Tanzania na kuipa nguvu zaidi dola ya Marekani z jambo ambalo linasababisha thamani ya dola dhidi ya sarafu nyengine duniani ikiwemo Tanzania.
Aidha, Waziri katika suala jengine ambalo pia linachangia kuagukakwa thamanio uya shilingi ya Tanzania ni Tanzania kutegemea zaidi fedha za wafadhili ambazo hutengwa kwa ajili ya kuendeshea miradi ya kitaifa.
Alisema fedha hizo zinapochelewa kuingizwa serikali hulazimika kuwa na mahitaji ya matumizi ya fedha za kigeni na hasa dola kuwa makubwa na husababisha kushuka kwa thamani ya shilingi.
No comments:
Post a Comment