Habari za Punde

Chaguzi za CCM Zaendelea Tawi la Tomondo


Na Hamad Hija-Maelezo Zanzibar 07/05/2012

Wanachama wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Tawi la Tomondo Wilaya ya Magharibi Mjini Zanzibar jana walifanya uchaguzi katika nafasi mbali mbali za tawi ambapo Hassan Kipanga Abdulla alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Tawi hilo.

Katika uchaguzi huo Hassan Kipanga Abdulla (Pomporipo) alichaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa tawi hilo baada ya kupata kura 116 na kumshinda mpinzani wake Said Ramadhan Nundu aliyepata kura 53.
  

Kufuatia matokeo ya uchaguzi huo msimamizi wa uchaguzi wa tawi hilo Waziri Omar Salim alimtangaza rasmi Hassan Kipanga Abdulla kuwa Mwenyekiti mpya wa tawi hilo la Tomondo  

Aidha katika uchaguzi huo wanachama walimchaguwa Hemed Ibrahim Masuod kuwa Katibu wa tawi hilo kwa kupata kura 35 na kumshinda mpinzani wake Khamis Hamza Abdulla aliyepata kura 22.

Nafasi nyengine iliyogombaniwa ilikuwa ya Katibu mwenezi ambapo katika nafasi hiyo Siajabuni Ali Mpate aliwashinda wapinzani wenzake kwa kupata kura 30 ambapo wapinzani wake Rose Merry alipata kura 24 wakati Mohd Ali Mpate aliambulia kura 4.

Katika uchaguzi huo uliofanyika kwa aman  na utulivu ulimchagua pia Amina Issa kuingia katika mkutano mkuu jimbo kwa kupata kura 90 na kumshinda mpinzani wake Benard Litope aliyepata kura 69.

Awali kulifanyika uchaguzi mwishoni mwa wiki hii ambapo Amri Said Hongo alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa Wazazi wa tawi hilo baada ya kupata kura 24 na kumshinda mpinzani wake Clementina Faustine Mapuri aliyepata kura 16 kati ya kura 44 zilizopigwa.

Kufuatia Hassan Kipanga Abdulla kuchaguliwa kuwa Mweyekiti mpya wa tawi la Tomondo kulimuwezesha kutoa shukurani kwa wanachama wenzake waliomuamini kumpa dhamana hiyo ya uongozi.

Kipanga alisema kuwa uongozi ni dhamana na hivyo kuahidi kuitumikia nafasi hiyo kwa moyo wake wote akiwa Mwenyekiti mpya wa Tawi la Tomondo.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR 07/05/2012

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.