Habari za Punde

CUF yatowa Tamko kuhusu vurugu - Yaitaka Serikali Kufanya Uchunguzi.

Na Juma Mohammed,MAELEZO
Chama cha Wananchi(CUF) kimewataka wananchi kutulia na Serikali kufanya uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha vurugu zilizotokea mwishoni mwa wiki Mjini Zanzibar.

Taraifa ya Chama hicho kwa vyombo vya habari iliyotiwa saini na Mkurugenzi wa Uenezi na Mahusiano na Umma,Salim Bimani ilisema “Chama cha CUF kinatoa wito kwa wananchi wote kuwa watulivu, wavumilivu na kuitumia fursa ya kutoa mawazo yao bila jazba na kutowanyima wengine nafasi ya kuwasilisha mawazo yao”

Taarifa hiyo ilisema kwamba vitendo vya watu wachache kuchoma makanisa moto na kuharibu mali za watu ni bvya uvunjifu wa sheria na kinyume na utamaduni wa Kizanzibari.

“Uchunguzi wa kina ufanyike na waliohusika wachukuliwe hatua za kisheria bila uonevu wala upendeleo” Alisema Bimani katika taarifa yake hiyo ambayo pia alisema kwamba ni lazima kwa wakati huu na kwa haraka iwezekanavyo, Serikali izungumze na Mashekhe bila ya kuona muhali na kwa uwazi kabisa ili kutafuta suluhu ya kudumu kwa faida ya nchi.

Chama hicho kimesema kwamba pamoja na sababu au visingizio mbalimbali vilivyotajwa kuwa chanzo cha hali hiyo, zikiwemo za hamasa za wananchi, chuki binafsi, ukosefu wa hekima,matumizi ya nguvu za dola na hata uchochezi wa makusudi wa wale wanaoonekana kutokupendelea maridhiano ya kisiasa Zanzibar.

“Chama cha Wananchi,CUF, kama sehemu muhimu ya Umma wa Watanzania,hakiwezi kukaa kimya kutokana na mwelekeo mzima wa hali tete ya amani katika nchi, ingawa ni dhahiri wapo baadhi ya watu wasioitakia mema Zanzibar wakibainika kufurahia mazingira hayo,kwa maslahi binafsi na pia kutoa kauli za kutatanisha za kisiasa” Alisema Bimani katika taarifa yake.

4 comments:

  1. Too little too late! CUF wanatuangusha bwana!
    Yaani wanaacha mpaka Wahuni wanakihusisha chama na hawa UWAMSHO ndio wanajidai kutoa kauli, tena baada ya CCM?

    Watu wasijisahau, wanacafu tumeshaumia sana hapa kwa kuhusishwa na misimamo mikali ya kidini, ikapelekea kuporwa ushindi mara kadhaa na kupigwa risasi za moto.

    Kwa mtu yeyote mwenye akili, anatakiwa ajue kwamba vurugu yoyote ya kidini ikitokea hapa CUF ndiwo watakao husishwa kwanza lakini viongozi wake wameamua kutia pamba masikioni.

    Dalili zote zinaonesha kwamba kuna usaliti ndani ya CUF-Z'bar ya kukiuwa chama watutie tena mitihani!

    Mambo hayaendi kabisa!..vyama vyote vikubwa sasa vina magazeti na mitandao CUF jiii!
    Ukiuliza wana mkakati gani wa kuimarisha chama Bara wanakwambia 'watu wa bara hawaaminiki' au wengine wanakwambia..ah sie twataka Z'bar yetu tu'..ah.. sasa wale watu wenu kule, waliokupeni viti viwili ya ubunge?.. na hivi sasa vijana kibao wa kiislamu wameamua kujiunga CUF japo haina uongozi imara..CUF..bwana! Mungu awasaisie!

    ReplyDelete
  2. Hili sio swala la cuf, hao cuf zamani wanajulikana km wamefunbwa midomo yao, sasa hivi kinachotakiwa ni zanzibar huru, tushachoka na ushenzi wa kitanganyika washenzi wakubwa, warudi makwao, na kama wataka kuisha znz watakuja na passport zao, washenzi.
    Tunataka nchi yetu, hatutaki muunganooooooooooooooooo,
    Tuawahieniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

    No wonder, they'll never leave us free because they need Zanzibar more than we need them.

    ReplyDelete
  3. Ukweli usemwe walochoma Makanisa wanajulikana, kuna tetezi kwamba mhusika au wahusika wakuu na walioshadidisha hayo wanajulikana na wala hawatokani na muamsho. Huo ni mkakati ulikuwa umeshapangwa kwa mda na walikuwa wakisubiriwa muamsho waandamane/wafanye matembezi yao tuu na wahusika wawamalize tena kwa fitna kubwa sana. Inasikitisha kuona taarifa ya naibu katibu mkuu ccm, zanzibar ilyojaa ukereketwa. Vuai, fikiria mbele ya safari.

    ReplyDelete
  4. Jamani ogopeni moto, hapa duniani ni sehemu ya kupita,viongozi wa Zanzibar munafanya dhulma hiyo,munawatesa watu kupata haki yao.Munawatumia wahuni kwa manufaa yenu ili nyinyi munenepe matumbo ya dhulma, jamani uongozi na ukubwa huo una mwisho wake.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.