Joseph Ngilisho, ARUSHA
WAZIRI wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe amewata wataalamu wa fedha, mawasiliano na uchukuzi kutafuta ufumbuzi wa tatizo la uduni wa miundombinu unaodidimiza uchumi barani Afrika.
Aliyasema hayo wakati akifungua mkutano wa mwaka wa Taasisi za fedha zinazofadhili maendeleo barani Afrika (AADFI), unaoenda sambamba na mkutano wa Magavana wa Benki ya Maendeleo Afrika unaofanyika Jijini Arusha.
Dk. Mwakyembe alisema mipango ya maendeleo na kukuza uchumi haiwezi kufanikiwa iwapo miundombinu haitaboreshwa ili kurahisisha usafirishaji.
Alisema hadi sasa nchi nyingi barani Afrika zinatumia barabara kama njia kuu ya usafirishaji badala ya reli ambayo licha ya kuwa na gharama nafuu lakini pia husafirisha kiwango kikubwa cha mizigo.
“Kukosekana na kutofanyia matengenezo ya mara kwa mara barabara zetu kunakwaza mawasiliano na hivyo kupunguza kasi ya kujiletea maendeleo kutokana na ukweli kwamba mawasiliano ndiyo nyenzo muhimu kiuchumi”, alisema Dk. Mwakyembe.
Alisema uduni wa njia za mawasiliano unachangia gharama kubwa ya usafirishaji ambayo humwangukia mtumiaji wa mwisho ambaye ni mwananchiwa kawaida anayelazimika kununua bidhaa kwa bei ya juu kulinganisha na wanaoishi kwenye nchi zilizoendelea kimiundombinu.
Dk. Mwakyembe alisema tatizo la miundombinu ni moja ya changamoto kwa serikali zote za Afrika katika juhudi za kukuza uchumi katika sekta zote ikiwemo kilimo ambacho ni uti wa mgongo kwa mataifa mengi, Tanzania ikiwemo.
Alitoa mfano wa Tanzania kwa kusema asilimia 95 ya mizigo mizito husafirishwa kwa njia ya barabara huku asilimia mbili pekee ikisafirishwa kwa reli na hivyo taifa kulazimika kutumia fedha nyingi kujenga na kukarabati barabara zinazoharibika mapema kutokana na kuzidiwa na matumizi.
Awali akimkaribisha Dk Mwakyembe, Mwenyekiti wa AADFI, Peter Noni alisema changamoto kubwa inayozikabili nchi za Kiafrika ni namna na njia bora za kumudu kujenga miundombinu za uhakika bila kutegemea misaada na ufadhili kutoka nchi wahisani na taasisi za fedha za kimataifa.
Noni ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Rasilimali (TIB), allisema miongoni mwa mambo yanayotarajiwa kujalidiliwa na kkutafutiwa ufumbuzi na namna ya kkutumia taasisi za fedha za ndani kugharamiaujenzi wa miundombinu kupitia mikopo yenye masharti nafuu.
No comments:
Post a Comment