Habari za Punde

Jamii Isifumbie Macho Vitendo vya Udhalilishaji wa Kijinsia

Laylat Khlafan
KUTOKANA na kushamiri kwa vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia, Wizara ya Ustawi wa Jamii, Wanawake na Watoto Zanzibar,imesema itawachukulia hatua kali za kisheria kwa wale wanaohusika na vitewndo hivyo.

Mkurugenzi wa Ustawi wa Jamii wa Wanawake na Watoto, Rahma Ali Khamis, alisema tatizo la unyanyasaji limeenea kila sehemu ambapo ngucvu ya pamoja inahitajika katika kulitokomeza hilo.

Mkurugenzi huyo alisema hayo katika ukumbi wa mkutano polisi Ziwani mjini Unguja wakati akitoa nasaha zake kwenye ufunguzi wa mafunzo ya siku tano, kuhusu uwendeshaji wa dawati la polisi la jinsia na watoto.

Alisema katika utafiti uliofanywa na Wizara hiyo, ulibainika kuwa vitendo vya udhalilishaji vinaanzia ngazi ya familia, majirani na hadi ngazi za juu hivyo kwa namna moja au nyengine udhalilishaji ni jambo ambalo, jamii imekuwa ikilifumbia macho na hivyo kuzidi kwa vitendo hivyo.

"Jamii yetu ibadilike na kwa kuwa bega kwa bega ili hawa wanaowanyanyasa watoto wafichuliwe, ili sheria iweze kufuata mkondo wake watawamaliza watoto", alisemaMkurugenzi.

Aidha alisema ili kuhakikisha jambo hili linakomeshwa lazima kuitumia elimu inayopatikana, kwa kufanya kazi pamoja, hasa kwa kuwaelimisha wale wanaoendeleza uhalifu huo.

Nae Mkuu wa kitengo cha mafunzo Polisi Tanzania, Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi Elice Mapunda, alisema anaamini kuwa mafunzo atakayoyafungua yataengeza uwezo wa jamii kufungua kesi za udhalilishaji wa kijinsia kwa upande wa jeshi la polisi.

Kwa upande wake, Mkuu wa chuo cha Taaluma cha polisi Zanzibar, Mkaribu Mwandamizi wa Polisi, Ramadhan Mungi, alieleza kwamba washiriki hao watajifunza mambo mbali mbali ikiwemo sheria za kitaifa na kimataifa juu ya haki za watoto,ukatili wa majumbani kuhoji waathiriwa wa vitendo vya ukatili.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.